Wachezaji wa Hispania wakishangilia ushindi baada ya kulinyakua Kombe la Mabingwa wa Ulaya
Timu ya soka ya Hispania imeifanyia unyama wa hali
ya juu timu ya Italia baada ya kuitandika mabao manne kwa bila katika mchezo wa
mwisho na hivyo kufanikiwa kutetea taji la Ubingwa wa Ulaya waliokuwa wakiushikilia
tangu 2008.
Mabao ya Hispania yalipachikwa kimiani na Silva
ndani ya dakika ya 14, goli la pili lilifungwa na Jordi Alba dakika ya 41. Msumari
wa tatu ulipigiriwa na mchezaji Ferdinand Torres katika dakika ya 84 huku
karamu ya magoli ikimaliziwa na Juan Mata katika dakika ya 88 kufuatia pasi
safi iliyopigwa na Ferdinand Torres.
Ushindi wa Hispania umetokana na juhudi za kutosha
zilizofanywa za kukaba ngome kuu za Italia zilizopelekea Balotelli kutofurukuta
na kuishia kuambulia nafasi ya pili. Refalii wa mech alichezesha kwa umakini wa
hali ya juu pasipo shaka dhidi yake.
Hispania wataendelea kulishikilia Kombe hilo la
Mabingwa wa Ulaya lenye uzito wa kilo sita kwa miaka mingine minne ijayo.
Timu ya Hispania iliyojazwa na wachezaji wa timu ya
Barcelona waliingia fainali mara baada ya kufanikiwa kuwaondosha Ureno katika
mpambano wa nusu fainali, huku timu ya Italia ikiingia fainali baada ya
kuibwaga timu ya Ujerumani.
Post a Comment