Kaimu afisa elimu mkoa
wa Iringa Euzebio Mtavangu akiwasikiliza wanafuni wa shule ya sekondari
Lyandembela Ifunda
WALIMU wa shule ya Msingi Hoho katika Manispaa ya Iringa waingia katika
kashfa nzito baada ya kutuhumiwa kuwachalaza bakora wazazi wa wanafunzi
wanaofika shuleni hapo kuhoji michango mbali Mbali .
Wakitoa malalamiko hayo mbele ya wanahabari waliofika shuleni hapo
kufuatilia Madai ya walimu hao kuendelea kuwachangisha wanafunzi michango isiyo
na risti .
Wazazi hao walisema kuwa uongozi wa shule hiyo umekuwa na tabia ya
kuwachangisha wanafunzi michango mbali mbali ikiwemo michango kwa ajili ya
mitihani ya kujipima kwa wanafunzi wa darasa la nne na Saba .
Alisema Zubeda Sanga kuwa pamoja na wazazi kuitikia wito huo wa kuwepo kwa
mitihani ya kujima kwa watoto wao ila bado uongozi wa shule hiyo umekuwa
ukichakachua michango hiyo na kushindwa kufanya kazi iliyokusudiwa .
Kwani alisema kuwa mbali ya uongozi wa shule hiyo kuwaagiza wazazi kutoa
michango hiyo ya shilingi 2000 kwa ajili ya kuchaposha mitihani hiyo ila fedha
hizo zimekuwa hazitumiki kwa kasi iliyokusudiwa badala yake zimekuwa zikitumika
kuwanufaisha walimu hao.
Alisema mitihani ambayo wanafunzi wamekuwa wakiifanya ni ile ambayo
ilifanywa na wanafunzi wa mwaka 2008 mitihani ambayo baadhi imechakaa kupita
kiasi na mingine imekuwa na panya na kunyeshewa na mvua.
Huku kwa upande mmoja Kati ya wazazi ambaye alipata kuadhibiwa kwa fimbo
shuleni hapo kwa Madai ya kuhoji uhalali wa michango hiyo Bw.Deus Kyando alisema
kuwa sababu ya kupigwa kwake na uongozi wa shule hiyo ni baada ya kufika shuleni
hapo na kuhoji michango hiyo.
Alisema kuwa baada ya kufika ofisi ya mkuu wa shule hiyo na kueleza sababu
ya ujio wake shuleni japo ndipo mkuu huyo wa shule alipofunga mlango na kuwaita
walimu wenzake na kuanza kumdhughulikia kwa bakora.
Hata hivyo alisema kuwa katakana na tukio hilo alilazimika kumjulisha ndugu
yake wa karibu kwa njia ya simu ila baada ya kufika naye aliidhia kupokea
kichapo kutoka kwa walimu hao.
Mzazi huyo alisema kuwa kutokana na ubabe wa walimu hao hivi sasa hata
akiitwa shuleni hapo kwa ajili ya kupewa taarifa ya mtoto wake amekuwa akiogopa
kwa kuhofia kichapo kutoka kwa walimu wa shule hiyo.
"Kiukweli sitakuja Kwenda tena shuleni hata nikaambiwa kuna jambo la
maendeleo kwa sababu hata nikifika shuleni ni nimekuwa nikiambulia
kichapo...sasa niende kufanya nini....afya yangu ni mbovu sana.....sasa Kwenda
shuleni kupigwa fimbo ni kutafuta mauti"
Aidha alisema kuwa suala la michango katika shule hiyo limeendelea kuwa
kero kubwa kwa wazazi na hivyo kuomba serikali kurejesha ada kuliko kuendelea
kutoa michango hiyo isiyo na utaratibu maalumu.
Mkuu wa shule hiyo hakuweza kupatikana ili kuthibitisha Madai hayo ya
wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
chanzo: Francis Godwin Blog
Post a Comment