Wanamuziki wa wa Bendi
ya DDC Mlimani Park
Waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma
Bendi mbili kongwe nchini, Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' na DDC Mlimani 'Wana Sikinde' wataoneshana ubabe mbele ya wabunge kesho katika Club Azizi, mjini Dodoma.
Akizungumzia juu ya mpambano huo, Msemaji wa Msondo Ngoma, Rajabu Mhamila, maarufu kwa jina la Super D, alisema kuwa shindano hilo la watani wa jadi litashuhudiwa na wabunge ambao kwa hivi sasa wanahudhuria vikao vya Bunge la Bajeti, mjini humo.
Wabunge na wapenzi wengine wa bendi hizo, watapata burudani safi kwa kupigiwa nyimbo mpya na zamani ambazo asilimia kubwa ya wabunge wanazikumbuka.
Alitaja baadhi ya nyimbo mpya zitakazopigwa na Msondo Ngoma kuwa ni; Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu, Suluhu ya Shaban Dede na Baba Kibene wa Eddo Sanga. pia zitapigwa nyimbo za zamani ili wabunge wajue wapi tulikotoka na wapi tulipo.
Baada ya shindano hilo, Msondo Ngoma Jumamosi watakuwa Baa ya Kontena Kibaha, mkoani Pwani na Jumapili watatoa burudani katika ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala, Dar es Salaam.

Post a Comment