
Dk. Faustine Ndugulile (pichani)
Naibu Spika Job Ndugai ameendelea kutema chche zake na safari hii rungu lake limemshukia Dk. Faustine Ndugulile kwa kuamulu atolewe nje ya ukumbi wa Bunge na asihudhurie vikao vitatu vya Bunge la bajeti linaloendelea kuunguruma huko Dodoma.
Mbunge Kigamboni Faustine Ndungulile alifukuzwa bungeni na kuzuiwa kuhudhuria vikao vitatu kwa kushindwa kuthibitisha rushwa wizara ya ardhi
Mbunge huyo wa kigamboni ametolewa nje na naibu spika Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake aliyoambiwa aifute kauli yake kwamba waziri amewahonga madiwani na kuwaleta Bungeni.
Na mapema ya leo Madiwani hao wa Kigamboni waliandika barua ambayo Naibu Spika, Job Ndugai ameisoma dakika chache kabla ya kufungwa kwa kikao cha asubuhi Bungeni leo, kuwa tuhuma walizorushiwa na Dkt. Ndugulile jana (alipokuwa akichangia bajeti ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), kuwa madiwani hao walipelekwa Bungeni baada ya kuhongwa na Wizara hizo.
Majina ya Madiwani hao na maeneo yao ya uwakilishi kwenye mabano ni: Dotto Msawa (Kigamboni), Albert Luambano (Tungi), Suleman Mathew (Vijibweni), Juma Nkumbi (Kibada).
Madiwani hao wanasema wanataka tuhuma hizo zithibitishwe na akishindwa kufanya hivyo awaombe radhi kitendo ambacho Ndugulile alishindwa kuthibitisha na hatimaye kufukuzwa Bungeni na Naibu Spika Job Ndugai
Post a Comment