Kamishina wa Idara
ya Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya Bw. Danford Makala (kulia)
akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Ustawi wa jamii wakati wa
mkutano kati ya Ujumbe wa Biashara na Uwekezaji
katika huduma za afya kutoka nchini Netherland na watendaji wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii jana jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu na
mmiliki wa Hospitali zinazojengwa kwa kutumia makontena (Hospitainer) na kuweza
kupelekwa kutoa huduma za afya maeneo yoyote kutoka
nchini Netherland Bw. Rolof Mulder akiongea na watendaji wa wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kuelezea namna kampuni hiyo inavyofanya kazi
zake.
Baadhi ya viongozi
wa ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini
Netherland wakifuatilia fafanuzi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa
na watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jana jijini Dar es
salaam.
Watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma
za afya kutoka nchini Netherland
Post a Comment