--
Mhe.
Spika,
Tarehe 27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania
(The Citizen) na nchi za nje (International news Agency – Bloomberg) viliandika
makala kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala
hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania
na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN.
Gazeti la “The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012
lilikuwa na kichwa cha habari “Iran Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo”
(meli za mafuta za Iran zinatumia bendera ya Tz kukwepa vikwazo.
TAARIFA YA ZMA
Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime
Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo
pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari
Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).
Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006,
kifungu no. 8 cha sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:
Section 8 (1). There shall be established the
registers of Tanzania Zanzibar ships to be Known as:-
(a). Tanzania Zanzibar International Register of
Shipping for ocean going ships; and
(b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for
coastal Ships.
(2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for
the purpose of this Act if that ship is registered under this
part.
Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama
ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za
kimataifa. (Open Registry).
Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na
mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za
mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.
Kama nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari
vimechapisha makala ya usajili wa meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN
kulingana na makala zao hizo.
SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta
ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake,
majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata
usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:
Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name
Ilikotoka
1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd
Malta
2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd
Cyprus
3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd
Malta
4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd
Malta
5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd
Cyprus
6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd
Malta
7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd
Malta
8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd
Malta
9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd
Cyprus
10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd
Cyprus
11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd.
Cyprus
Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons Meli hizi ni 11 kama
zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi
zinazobadilisha usajili wao (De registration).
Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na
Malta. Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine
20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha
usajili wao na kwenda usajili wa “TUVALU Islands”.
ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita
wenye meli hizi na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au
makampuni ya mafuta ya IRAN.
Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis
tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza
kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua
kuja kusajili meli
ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili
wetu wa nje (Open Registry). Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza
kwamba ikiwa ZMA haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta
usajili wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine
(PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na
Malta.
Kinyume na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari
juu ya uraia wa wamiliki wa meli hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza
katika usajili wa meli zao wana uraia wa British Vergin Islands na Sychelles.
Kulingana na “United Nations Convention Law of the Sea”, Article 91, na za
“Geneva convection of Registration” articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar
Maritime Transport Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya
nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili
meli yeyote kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa
zinazoongoza usajili huo.
Maelezo haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi
kuwa Zanzibar imesajili meli za IRAN ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na
nchi za Umoja wa Ulaya (European Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta
kutoka Iran.
Mhe. Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina
madhumuni yeyote zaidi ya kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka
kusajili meli zao kwetu.
Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili
uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba
Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli
mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya
nchi.
Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika
kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa
zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine
zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi
wake.
Hata hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa
kitaifa na kimataifa katika biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli
zinasajiliwa chini ya mamlaka hii zinafata taratibu ilizoweka.
Mhe. Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya
habari (The Citizen), Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe)
alipokuwa akijibu suala Bungeni hivi juzi hakuonyesha kurishiki kwake katika
usajili wa meli (Open Registry) inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara
ya kuja Zanzibar kuonana na Waziri anaehusika kuzungumzia suala
hili.
Taarifa za “The Citizen” zaweza kuwa ni muendelezo wa
Mhe. Mwakyembe kutoridhika kwake katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia
uwakala wake huko Dubai. Mhe. Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi
yeyote.
Hili ni suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali
yetu ni njia moja ya kuongeza mapato yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili
huo hauvunji sheria za Kimataifa.
Mhe. Spika, Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda
mrefu na nchi nyingi ikiwemo IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni
(Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani
IRAN itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo.
Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio
vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu. Hivyo, kwa taarifa
hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo vya habari kuhusiana na suala
hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo juu. Mhe. Spika, naomba
kuwasilisha.
Hamad Masoud Hamad
WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
ZANZIBAR
chanzo: Kamanda wa Matukio Blog
Post a Comment