Balozi wa
Marekeni Alfonso Lenhardt akiwa katika picha ya pamoja na watu wanaoishi
na virusi vya UKIMWI wanaopata huduma zao katika kituo cha Alamano, cha
mjini Iringa.Picha na Frank Leonard-Habari Leo
---
Mratibu wa Kituo hicho, Christopher Kunzugala alisema Jumuiya za Kuweka na Kukopa (SILC) katika kituo hicho zina hisa zenye thamani inayokadiriwa kufikia Sh milioni 200, huku hisa moja ikiuzwa kati ya Sh 500 na Sh 10,000 kwa wanachama wa vikundi 52 vilivyoanzisha jumuiya hizo.
Balozi
Lenhardt alisema Watu wa Marekani kwa kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani
wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) walianza kukisaidia kituo hicho tangu
kilipoanza kutoa huduma ya uangalizi na matibabu mwaka 2005, “Kituo
hicho si tu kwamba kinawapa watu fursa ya kupata huduma ya upimaji na
matibabu, lakini pia kinatoa huduma za uangalizi na misaada kwa watu
wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI,” alisema.
Alisema
ushirikiano wao na kituo hicho umewezesha mpaka sasa Marekani isaidie
utoaji huduma ya uangalizi na misaada kwa watu watu 2,043 wanaoishi na
virusi na watu 1,795 wanaopata huduma za matibabu kituoni hapo. Aidha
alisema kupitia misaada ya Watu wa Marekani, programu za “Tunajali na
Pamoja Tuwalee”, wametoa mafunzo kwa waelimisharika majumbani 85.
Mkurugenzi wa Kituo cha Alamano, Maria Mikela alisema kituo kimejengwa
kupitia Programu ya Awamu ya Pili ya Mradi wa Tunajali unaofadhiliwa na
USAID.


Post a Comment