Chama
cha Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi (TARPOA) kinatarajia kufanya
Mkutano wake wa kwanza Septemba 29 mwaka huu katika Chuo cha Taaluma za
Polisi Kurasini kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kulsaidia Jeshi la Polisi katika kukabiliana na uhalifu.
Hayo yalisemwa Mwenyekiti wa
TARPOA, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Bw.Hilal Rashid wakati
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
kuhusiana na mkutano huo ambao utawakutanisha wastaafu wote wa Jeshi la
Polisi .
Kamishna Mstaafu Rashid alisema
malengo ya kuanzisha Chama hicho nikuwaunganisha wastaafu wote wa Jeshi
la Polisi na hatimaye kuwaendeleza katika nyanja mbalimbali ili waweze
kuutumia uzoefu wao katika kuhakikisha amani na usalama vinadumu hapa
Nchini.
Aidha alitoa wito kwa Askari
wastaafu wote wa Jeshi la Polisi kujiunga katika Chama hicho kwakuwa
kitawasaidia katika kupata maendeleo na kulisaidia Taifa kwa taaluma
walizonazo.
Kwa Upande wake Msemaji wa
Jeshi la Polisi Nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi Bi. Advera Senso
alisema Chama hicho ni muhimu sana kwa kuwa kitalisaidia Jeshi la Polisi
hasa katika Dhana yake ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi
kwakukizingatia wastaafu hao wanauzoefu katika nyanja ya ulinzi na
usalama .
Bi Senso alisema wao kama Jeshi
la Polisi watafanya kazi na TARPOA na watashirikiana nao kwa kuwa
wanatambua mchango wao katika kipindi chote walicholitumikia Jeshi hilo
mpaka hivi sasa.


Post a Comment