Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WASANII WAASWA KUVUTIA WATALII NCHINI


WASANII  sanaa za maonesho nchini wamepewa changamoto ya kutambua kuwa watalii ni hadhira ambayo wanaweza kuilenga katika ubunifu wa  kazi zao ili kuweza kukuza utalii wa kiutamaduni ambao utasaidia kuongeza mapato kwa ajili ya maendeleo yao na taifa zima.
kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni(TAsuBA) Juma Bakari wakati  akiwalisisha mada ya ‘Sanaa za Maonesho kama Kivutio cha Utalii Tanzania’ wakati wa kongamano la Tamasha la 31 la Sanaa na Utamaduni lililofanyika kwenye uwanja wa taasisi hiyo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Alisema sanaa za maonesho ni kivutio kikubwa cha cha utalii ni muhimu  wasanii  kuwa  na mtazamo huo ili kuangalia fursa zilizopo. Lazima watambue watalii ni hadhira ambayo wanaweza kuwalenga kwa kuwafahamu kwa makundi.
Alitolea mfano kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 sekta ya utalii imeingiza mapato makubwa na imekuwa chanzo cha mapato ya fedha za kigeni,ambapo nchi yetu ilipata dola za Marekani bilioni 1.8 na inatarajia kupata  dola za Marekani  bilioni tatu ifikapo mwaka 2015.
Aliongeza kuwa ni vizuri wasanii hao wakajifunza kutoka kwa wenzao wa Kenya na Uganda ambao wamefanikiwa kuhamasisha utalii huo kwa kutumia ngoma na muziki wa asili.
Mkuu huyo wa taasisi hiyo alisema Lugha ya Kiswahili inaweza kuwa ni kivutio cha watalii ikiwa wasanii hao watatayarisha tamthilia za lugha  kwa maneno mepesi.
Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili  katika kukuza utalii huo, alisema zaidi ya vikundi 4000 vilivyosajiliwa ,hakuna hata kimoja kinachoonyesha kukuza utalii huo. Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa elimu ya biashara na ujasiriamali hali inayosababisha vikundi vingi kutegemea wafadhili  hatimaye kuanzishwa halafu vinakuwa havipo.
Aidha alifafanua kuwa kampuni za kitalii nazo zinachangia kutokuza utalii huo kwa kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili za mwaka 2011-2012 kampuni hizo ziko 385, kati ya  hizo 85 ni za kigeni . Pia kulingana na utafiti uliofanywa hata zilizobakia zinaendeshwa na wageni  ambao sio jambo rahisi  kwa wao kuukuza kwa vile hawaufahamu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top