---
Chama Cha Mapinduzi ,Tawi la Uingereza Jana Tarehe 09.09.12 kimefungua
shina Jipya katika Mji wa Leicester kwa changamoto ya hali ya juu, hoja nzito na
kishindo kikubwa.
Katika ufunguzi huo uliosimamiwa na
Katibu Mpya wa Tawi Bi. Mariam Mungula alisisitiza suala la umoja kwa wana CCM
na wanadiaspora kwa ujumla katika kutoa mchango wao kwa sauti moja ili kuweza
kuwa na Nguvu ya pamoja na kuchangia katika
kuboresha ufanisi wa Serikali ya Tanzania kwenye Nyanja mbali mbali za
huduma za kijamii na maendeleo ya kiuchumi kwa faida ya watanzania wote.
Awali Bi. Mungula alitoa salamu
kutoka kwa Mh. January Makamba kama Katibu wa NEC Siasa na Ushirikiano wa
Kimataifa ambae aliwahakikishia wana CCM Diaspora kuwa , CCM huko nyumbani
,akiwemo Mwenyekiti wa Taifa ,Mheshimiwa Jakaya Kikwete inathamini sana imani
ya wanachama wa Diaspora na kazi wanayofanya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Mh. January Makamba aliahidi wana Diaspora kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaweka
mfumo mzuri ili kuyatumia mawazo ya wana CCM walioko nje ya Nchi ili kukiimarisha Chama.
Viongozi wa Shina Jipya la CCM
Leicester waliochaguliwa ni kama wafuatavyo:
- Cletus Shigela – Mwenyekiti
- Moses Kusamba – Katibu
- Hussein Hussein – Mjumbe
- Pauline Nzengula – Mjumbe
- Agness J Nyehunge - Mjumbe
6. Mzee Khalid Kassim Ndagiye
(Mlezi)
Katika ufunguzi huo ambao
ulihudhuliwa na wana Leicester wengi , hoja mbalimbali katika masuala ya
kukiendeleza chama katika utawala wa nchi zilijadiliwa na kutolewa ufafanuzi na
viongozi wa Tawi akiwemo Mh. Haruna Mbeyu “Special Advisor”, Bw. John Lyimo -
Uchumi na Fedha, Bw. Abraham Sangiwa Naibu Katibu Uenezi na Siasa Tawi na Bw.
Albert Ntemi Naibu Katibu Tawi.
Baada ya mahojiano na Uongozi wa
Tawi na kujibu maswali yaliyokuwa
yakiwasumbua wanachama, wakereketwa na makada wengi , wanachama wapya wengi
walijitokeza na kujiunga na CCM papohapo na kukabidhiwa Kadi za uanachama na
Katibu wa Tawi Bi. Mungula,huku wakishangiliwa na kupongezwa na wanachama
wenzao na uongozi mpya wa Tawi la CCM UK. Waliobaki katika wahudhuriaji hao
walishakuwa na kadi za Chama Cha Mapinduzi zamani na hivyo walionyesha furaha
kubwa kuwa sasa wataweza kuzitumia kadi zao baada ya kuwa na Shina katika mji
wao.
Kabla ya uchaguzi wa viongozi wa
shina jipya ambao uliendeshwa kwa demokrasia ya hali ya juu, akijibu hoja za wana Leicester Naibu Katibu wa
Siasa na Uenezi wa Tawi Bw. Abraham Sangiwa aliwakumbusha wajumbe kuzifahamu
haki, sifa na wajibu wa uanachama na miiko ya uongozi kama ilivyoainishwa
katika miongozo na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.
Kidumu
Chama Cha Mapinduzi
Mariam
Mungula
Katibu wa Tawi la Chama Cha
Mapinduzi, Uingereza
CHAMA
CHA MAPINDUZI -UK.
Imetolewa na Idara ya Siasa na
Uenezi, Tawi la CCM ,Uingereza.
Tarehe: 10 Septemba 2012.
Post a Comment