CHAD DAWSON AKIWA CHINI BAADA YA KUTWANGWA NA ANDRE WARD
Andre
Ward amemtwanga Chad Dawson na kutetea mikanda yake ya WBC-WBA Super
Middle weight katika pambano lililopigwa Oakland California.Ilikuwa ni pambano la kukata na shoka kutoka kwa bingwa mara sita ambaye alikuwa anashikilia mkanda wa WBC chad dawson.
Andre ward alimwangusha chini Dawson katika raundi ya tatu na mwanzo wa raundi ya nne na kudhibiti kabisa pambano lote na hatimaye kumaliza pambano zikiwa zimebaki sekunde 15 kukamilisha raundi ya 10. kwa ushindi huo ward amekuwa na rekodi ya 26-0 akiwa ameshinda mapambano 14 kwa aina ya knock out wakati Dawson ameshuka kwa mapambano 31-2.
Hivi ndivyo tulivyokuwa tunataka alisema Ward, katika boxing watu wanaangushwa sana kwa knockout.kila mtu anapenda kushinda kwa knockout,niliwaambia watu nataka kushinda lakini si lazima kwa knockout lakini linapokuja suala la knockout ni jambo zuri sana.
Post a Comment