Wachezaji na Viongozi wa Young Africans wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda cha bia TBL - Dar es salaam
Bwana Sawe akitoa maelezo jinsi ya bia inavyochujwa kwa wachazaji na viongozi wa klabu ya Yanga
Wachazaji wa Yanga wakipata maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa TBL bwana Sawe
Mabingwa
wa Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati, timu ya
Young Africans imnefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza bia
TBL kilichopo eneo la mchikichini Ilala.
Young
Africans imefanya ziara hiyo ikiwa ni taratibu zilizowekwa na kampuni
ya TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro ambao ndio wadhamini wakuu
wa timu ya Yanga.
Ziara
hiyo ilianzia kwa kutembelea sehemu ya uchambuaji wa vimea, kisha
kupita sehemu ya kuanda na kuchemsha vimea, ambapo walipata maelezo
mazuri kutoka kwa Sawe ambapo wachezaji na viongozi walionekana kuelewa
zaidi maelezo yake.
Sawe
aliwalezea taratibu za kuandaa bia katika kiwanda hicho, ambapo alisema
kiwanda hicho kinatengeneza bia aina 14 ambapo kiwanda cha Dar es
salaam, ndio kinaongoza kwa uzalishaji, kiifuatiwa na Mwanza, Arusha na
Mbeya.Kocha Tom Saintfiet alisema amefurahi sana kupata nafasi hiyo
pamoja na wachezaji wake kutembelea kiwanda cha bia, ambapo alisema
anashukuru kampuni ya TBL kupitia bia ya kilimanjaro kuwa wadhamini wa
mabingwa wa soka afrika mashariki na kati.
Wachezaji
pia walipita sehemu ya uchachushaji wa togwa, kabla ya kupita sehemu ya
kuchujia bia na kisha kuendelea na sehemu ya upakiaji bia kwenye chupa,
ufungwaji wa vizibo kwenye chupa na kisha sehemu ya kupakia kwenye
makreti na kufungwa kweye maboksi kwa bia za makopo.
Utembeleaji
huo wa kiwanda ulitumia masaa zaidi ya mawili na baada ya hapo, TBL
iliandaa vitafunwa na vinywaji kwa ajili ya wachazaji na Viongozi wa
Yanga, huku wafanyakazi wa TBL wakijumuika pia katika hafla hiyo.
Akiongea kwa niaba ya uongozi, Afisa Habari wa Yanga Louis Sendeu
alisema tunashukuru TBL kwa kutupa mwaliko wa kuja kujionea jinsi bia
inavyoandalia mpaka kufikia hatua ya mwisho ya kutumiwa na mteja, kwa
kweli ni faraja sana na kukupitia wadhamini wetu bia ya Kilimanjaro,
tunasema ahsanteni sana na sisi tunaahidi hatutawaangusha katika
kuitangaza kilimanajaro kwa kufanya vizuri katika michezo yetu ya ligi
kuu Tanznaia itakayoanza wiki ijayo alisema "Sendeu"
Kocha
Tom Saintfiet alisema kwa kweli ziara imekwua nzuri, mimi nimefurahi
kutemmbelea kiwanda cha wadhamini wetu na wachezaji wangu kwa ujumla na
benchi la ufundi tumefurahi, hatuna cha kusema sana zaidi ya kuwaahidi
kuendelea kuitangaza bia ya kilimanajaro kimataifa.
Meneja
wa bia ya kilimanjaro Geroge Kavishe aliishukuru Yanga kwa kuja
kutembelea kiwanda na pia kwa kuitanagza bia ya kilimanajro nje ya
mipaka ya Tanzania, ambapo katika ziara ya maandalizi ya ligi nchini
Rwanda kupitia Yanga bia ya kilimanjaro imepata wateja wengi na
wanfaikiria hivi karibuni kuanza kupeleka kinywaji hicho huko.
Timu
ya Yanga inatarajiwa kusafiri kuelekea Jinjini Mbeya katikati mwa wiki
ijayo, kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara ,
ambapo katika mchezo wa ufunguzi itacheza na wenyeji timu ya Tanzania
Prisons tarehe 15 septemba 2012 katika Uwanja wa Sokoine.
Post a Comment