Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kimemfungulia kesi Mahakama Kuu Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye, kutokaa na madai yake kwamba Chadema wanapewa mabilioni ya fedha
na mataifa tajiri.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willibroad Slaa, alisema hayo jana wakati wa
semina ya viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama wa Chama cha
Christian Demokratic Union (CDU) cha Ujerumani.
Semina hiyo kuhusu Uhuru, Demokrasia na Mshikamano inawashirikisha
baadhi ya wabunge na viongozi wa Kamati Kuu ya Chadema ambapo wanajadili
masuala ya kukuza uchumi wa soko unaoshirikisha watu wenye kipato cha
chini na juu ambao unaleta dhana ya uwajibikaji kwa taifa na serikali.
Dk. Slaa alisema Chadema kimemfungulia kesi namba 186 /2012 Nape ili
aweze kuthibitisha madai yake kwamba chama hicho kinapata mabilioni ya
fedha toka kwa mataifa tajiri.
Alisema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia propaganda ambazo zimekuwa
zikielezwa na baadhi ya watu kuwa Chadema wanapata mabilioni ya fedha
kutoka nje wakati hakuna ukweli wa suala hilo.
“Ipo propaganda kuwa chadema inapata mabilioni ya fedha toka nje,
kimsingi, marafiki zetu kama Konrad Adenauer Stiftung wanatusaidia kwa
ajili fedha za kujengea uwezo, lakini siyo kwa ajili ya kuendesha
kampeni au shughuli za kiasiasa,” alisema Dk. Slaa.
Chadema hivi karibuni walimtaka Nape kukiomba radhi chama hicho pamoja
na kutoa Sh. bilioni tatu, baada ya kudai kuwa Chadema kinapata
mabilioni ya fedha toka mataifa ya nje ambapo alikataa kuomba radhi kwa
kueleza tuhuma alizitoa dhidi ya chama hicho ni za kweli.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema mifumo ya uchumi katika
nchi yeyote inategemea itikadi na sera ya nchi. lakini serikali ya CCM
inaegemea ujamaa na kujitegemea ilhali sekta za uchumi zipo chini ya
soko huria.
Alisema kwa Chadema inafuata mlengo wa katikati ambapo imechukua yale
mazuri ya mfumo wa ujamaa na kujitegemea na kuchanganya na sera ambazo
zinalenga kumwinua mwananchi kiuchumi.
Loading...
Post a Comment