Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DOWANS YAIBWAGA TENA TANESCO

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kusema kuwa amekubaliana na hoja za wakili wa wadaiwa (Dowans), Kennedy Fungamtama.
Katika kesi hiyo TANESCO ilikuwa ikiwakilishwa na mawakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza, Lugano Mwandambo, Dk. Eve Hawa Sinare, Dk. Ale Nguluma na Majura Magafu.
Alisema mahakama haiwezi kusikiliza ombi hilo kwa sababu tayari TANESCO walishawasilisha Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi, Septemba 28 mwaka 2011 iliyoruhusu tuzo hiyo isajiliwe.
Jaji Twaib alisema kabla ya kutoa uamuzi huo alijiuliza kama mahakama ina mamlaka ya kukubali ombi la TANESCO lililotaka mahakama hiyo izuie utekelezwaji wa ukazaji hukumu kwa sababu tayari imeshawasilisha hati ya nia ya kukata rufaa ya hukumu ya Jaji Mushi.
Alisema katika uamuzi wake ameona mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza ombi hilo na kuongeza kuwa, ilikuwa na mamlaka ya kulikubali kabla TANESCO haijawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu iliyoruhusu usajili wa tuzo ya Dowans.
“Kwa kuwa tayari TANESCO walishawasilisha Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudia la kukata rufaa kupinga hukumu ya mwaka 2011 ya Jaji mstaafu Mushi… Mahakama Kuu, hapo mamlaka yake ya kukubali ombi la TANESCO la kutaka Dowans isikaze hukumu ya Jaji Mushi nguvu hizo zinakufa na kwa maana hiyo maamuzi ya Jaji Mushi hadi leo hii bado hayajatenguliwa,” alisema.
Kutokana na hoja hiyo, alisema anatupilia mbali ombi hilo na kwamba hatatoa amri ya kuitaka TANESCO ilipe gharama.
Septemba 28 mwaka 2011, Jaji Mushi alitupia mbali ombi la TANESCO lililoomba tuzo iliyotolewa na Mahakama ya ICC kwa Dowans isisajiliwe hapa nchini na akaruhusu isajiliwe kwa sababu uamuzi wa Mahakama ya ICC ulikidhi matakwa ya kisheria.
Novemba 15 mwaka 2010, Mahakama ya ICC iliipatia tuzo ya ushindi Dowans  ya dola 65,812,630.03 za Marekani baada ya TANESCO kukutwa na hatia ya kuivunjia mkataba kinyume na mkataba.

Chanzo: Tanzania Daima


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top