Kutokana
na kuendelea kwa mfululizo wa matukio mbalimbali yanayosababishwa na
vurugu za kisiasa kati ya baadhi ya vyama vya siasa dhidi ya jeshi la
polisi, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania imesema imechoshwa
na matukio hayo ambayo yamekua yakisababisha vifo vya mara kwa mara kwa
raia wasio na hatia.
Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amesema ofisi yake kuanzia sasa
imepanga kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kukifuta chama chochote
cha siasa kitakachothibitika kufanya mkutano kinyume cha sheria na
kusababisha vurugu pasipo kujali kama vurugu hizo zimedhuru au
hazijadhuru raia yeyote.
Vilevile Tendwa amekemea kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa nchi
nzima na baadhi ya vyama vya siasa na kupewa jina la ‘OPARESHENI’ ambapo
amedai kuwa huu si wakati wa vyama kuanza kampeni, hivyo chama chochote
kitakachoendelea na kampeni kwa mtindo huo kuanzia sasa kitachukuliwa
hatua kali ikiwemo kukifutia usajili.
Post a Comment