Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa
hotuba fupi ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,
Fanuel Mbonde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya kukabidhi
mabasi kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Fidelis Mboya kwa niaba
ya Jeshi la Magereza. Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria iliyopo
ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria imekabidhi magari 12 kwa Jeshi la
Magereza kwa ajili ya kubeba mahabusu pamoja na kusindikiza msafara wa
mahabusu wanapopelekwa mahakamani na kurudishwa gerezani. Hafla hiyo
imefanyika jana katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (Watatu
kutoka kulia waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,
Fanuel Mbonde (Wanne kutoka kushoto waliokaa) pamoja na Maofisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kusafirisha mahabusu pamoja na
magari madogo ya kusindikiza msafara wa mahabusu hao wakati
wanapopelekwa Mahakamani na kurudishwa Gerezani. Hafla hiyo imefanyika
katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu
Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akipokea
funguo ya basi la mahabusu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Fanuel Mbonde katika fupi ya kukabidhi mabasi kwa Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza, Fidelis Mboya kwa niaba ya Jeshi la
Magereza. Programu ya Maboresho katika Sekta ya Sheria iliyopo ndani ya
Wizara ya Katiba na Sheria imetoa magari madogo matano na mabasi saba
kwa ajili ya kusafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na
kurudi Gerezani. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jana katika
viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa pili
kutoka kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel
Mbonde (wa tatu kutoka kulia) wakikagua sehemu ya magari madogo
yaliyokabidhiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusindikiza
msafara wa mabasi yanayosafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda
Mahakamani na kurudi Gerezani.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (Wa kwanza
kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (Wa
pili kulia) wakikagua sehemu ya mabasi makubwa yaliyokabidhiwa na Wizara
ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusafirisha Mahabusu kutoka Gerezani
kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani. Kulia ni Mratibu wa Programu ya
Maboresho katika Sekta ya Sheria, Emmanuel Mayeji.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
on Wednesday, September 26, 2012
Post a Comment