Muungano
wa Ulaya (EU) umeamua kusitisha misaada kwa Rwanda, uamuzi huo
umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo iliyodai
kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo.
Waasi hao wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Pamoja
na Rwanda kuendelea kukana madai hayo, mwezi Julai Marekani pia ilizuia
dola 200,000 zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda.
Post a Comment