Hayo yalisema na wajasiriamali hao katika risala yao iliyosomwa mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda jijini Mbeya jana katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali Nyanda za Juu Kusini yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo (Sido).
Katika risala hiyo iliyosomwa na Rhoida Mwazembe, wananchi hao waliiomba serikali kuhamasisha Watanzania kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari.
Akijibu risala hiyo Kigoda alisema kuwa serikali inashughulikia tatizo la upatikanaji mgumu wa mitaji kwa wajasiriamali hao.
Kigoda alitoa agizo kwa Halmashauri zote za wilaya nchini kuhakikisha zinatenga haraka maeneo maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao.
Aliongeza kuwa serikali inatambua umuhimu wa sekta hiyo kwa kuwa inakuwa kwa kasi hivyo itajitahidi kuondokana na nadharia na kufanya mambo kwa vitendo zaidi.
chanzo: Tanzania Daima
Post a Comment