|
Watuhumiwa wa vurugu
za Mbagala wiki iliyopita, wakiwa chini ya ulinzi wa polisi, walipofikishwa
mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza jana.
Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali
kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki
iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu,
kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana ya watu hao
itaamuliwa Oktoba 30.
|
Baadhi ya
watuhumiwa wa vurugu zilizotokea Mbagala jijini Dar es Salaam
wiki iliyoipita, wakiwa ndani ya gari la polisi walipofikishwa mahakama
ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Oktoba 16, 2012 kwa mara ya
kwanza. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka
mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto
wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa
waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana
ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30. |
|
Akina mama
wanaotuhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea huko Mbagala, wilayani Temeke
jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, wakishuka kutoka ndani ya gari la
polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.
Akina mama hao ni miongoni mwa watuhumiwa 29 waliofikishwa kwenye mahakama
hiyo kujibu mashtaka ya kuhusika na vurugu za kuvamia makanisa, kuchoma,
kuharibu mali na
kuiba. |
|
|
Polisi aliyejihami
kwa bunduki na radio ya mawasiliano, akishika doria kwenye lango la kuingilia
chumba cha mahakama ambako watu 29 walifikishwa mahakamani hapo Jumanne
Oktoba 16, 2012, wakikabiliwa na mashtaka kadhaa ya kuvamia makanisa,
kuharibu, kuiba na kuchoma mali za makanisa hayo wiki iliyopita huko Mbagala
jijini Dar es Salaam. Wote wamerejeshwa mahabusu hadi Oktoba 30 ambapo
mahakimu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo, wameahidi kutoa uamuzi juu ya
hatma ya dhamana |
on Wednesday, October 17, 2012
Post a Comment