…………………………………………………………
Viongozi na watu wenye maono katika kukuza Uboreshaji wa Kilimo Afrika (Green Revolution) jana usiku walituzwa katika Baraza la Uboreshaji wa Kilimo barani Afrika (African Green Revolution Forum (AGRF)) (http://www.agrforum.com) katita chakula cha jioni cha tamasha la kutoa tuzo mjini Arusha. Tuzo za AGRF zinawatambua viongozi wa ngazi za juu wa Afrika katika jitihada za kuhamashisha watu juu ya mipango ya ya uma naya kibinafsi ili kujenga tasnia edelevu ya kilimo biashara barani Afrika, kutia msukumo katika Uboreshaji wa Kilimo na kuwezesha Afrika kuwa na lishe bora na chakula cha kutosha.
Watu na mashirika yafuatayo yaliheshimiwa kwa kujitoa na kufanya kazi bora katika nyanja zifuatazo:
• Habari na Uadishi– Joshua Kato, Uganda
• Mashirika ya Sekta ya Kibinafsi– Neema Agricole du Faso (Nafaso), Burkina Faso
• Mashirika ya Wakulima– Faso Jigi, Mali
• Taasisi za Elimu na Utafiti–The African Centre for Crop Improvement, at the University of KwaZulu – Natal, South Africa; and Makerere University, Uganda
• Mashirika ya Utetezi– Rural Urban Development Initiatives (RUDI), Tanzania
• Vijana na akina Mama– Africaworks, Mozambique
Dr. Namanga Ngongi Apokea Tuzo la Fanikio la Maisha (Lifetime Achievement Award)
Tuzo la AGRF la Fanikio la Maisha lilitolewa kwa Dr. Namanga Ngongi kwa mchango wake katika kugeuza sekta ya kilimo Afrika. Dr. Ngongi ana uzoefu mwingi katika Nyanja za kilimo na usalama, kuanzia nchini mwake Kameruni, alimofanya kazi kama afisa wa kilimo nyanjani katika Wizara ya Kilimo, akisaidia wakulima kuboresha na kupanda mazao mbalimbali na kuyauza. Baadaye alitumikia majukumu kadhaa: alifanya kazi katika Ubalozi wa Kameruni kule Roma, alitumika kama Naibu Mtendaji wa Shirika la Chakula Duniani, na aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu na Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Misheni ya Kuleta Amani ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Dr. Ngongi alikuwa Rais wa kwanza wa kudumu wa Ushirikiano kwa ajili ya Uboreshaji wa Kilimo (AGRA), na kustaafu mwaka wa 2011.
Tuzo la YARA la 2012 Lilitunukiwa Viongozi wa Kike wa Kiafrika
Kilele cha tamasha la tuzo za AGRF kilikuwa tuzo la YARA – Shidano Kubwa la mchango wa kipekee wa kuimarisha ukuaji wa ukulima na usalama wa chakula Afrika, na kuongoza Uboreshaji wa Kilimo katika Afrika wa kuongozwa na Waafrika.
Shirika la Kimataifa la Yara (Yara International) lilimtunukia Tuzo la Yara 2012 Dr. Agnes Kalibata, Waziri wa Kilimo na Rasilmali za Wanyama wa Rwanda na Dr. Eleni Gabre-Madhin, Mkurugenzi Mkuu anayeondoka wa Halmashauri ya Ubadilishanaji wa Bidhaa (Ethiopian Commodity Exchange) nchini Ethiopia. Dr. Kalibata na Dr. Gabre-Mahdin walitunikiwa tuzo la Yara kwa kazi yao katika maeneo ya uanzilishi wa Uboreshaji wa Kilimo Afrika.
Dr. Kalibata alitambuliwa kwa uongozi wake wa kipekee katika mageuzi ya usalama wa chachula na maendeleo ya kilimo nchini Rwanda.
Dr. Gabre-Mahdin alituzwa kwa utumishi wake uliyotambulika katika utaratibu wa mageuzi yaliyoleta ubora wa soko, hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa kahawa nchini Ethiopia.


Post a Comment