THE UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
JK:
Naridhishwa na Kazi ya Tume ya Katiba
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema
kuwa anaridhishwa na mwenendo mzima wa kazi ya Tume ya Kukusanya na Kuratibu
Maoni ya Wananchi Kuhusu Katiba.
Aidha,
Rais Kikwete amewataka wajumbe wa Tume hiyo kuwakumbusha wananchi kutokutoa
maoni kwa kutumwa na watu wengine bali watoe maoni yao wenyewe kwa kadri
wanavyotaka Katiba yao mpya iwe.
Rais
Kikwete ameyasema hayo leo, Jumanne, Oktoba 30, 2012, kwenye Ikulu Ndogo mjini
Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro wakati alipokutana na kuzungumza kwa muda mfupi na
baadhi ya wajumbe wa Tume hiyo wakiongozwa na Profesa Baregu Mwesiga ambao
walikwenda kumjulia hali Rais. Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu
katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Wajumbe
hao wanne ambao walikutana na Rais Kikwete ni sehemu ya wajumbe wa Tume ambao
wako mkoani Kilimanjaro kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi wa mkoa huo
kuhusu Katiba. Watakuwa Kilimanjaro hadi tarehe 6 Novemba, 2012.
Rais
Kikwete amewaambia wajumbe hao: “ Kwa maoni yangu nadhani kazi ya Tume
inakwenda vizuri na mimi nawatakia kila heri katika shughuli hii muhimu kwa
mustakabali wa taifa letu. Zitakuwepo changamoto, lakini hizo hazikosi katika
shughuli yoyote ya binadamu.”
Aliongeza
Rais Kikwete: “Nawaomba tu muendelee kuwaelimisha wananchi
kuwa ni vizuri kwao kutoa maoni yao wenyewe siyo kwa kutumwa na watu wengine.
Wahasishwe wasiwe kaseti za kucheza maoni ya watu wengine.”
Profesa
Baregu amemwambia Rais Kikwete kuwa kazi ya Tume hiyo inakwenda vizuri na
wajumbe wa Tume wanayo matumaini makubwa kuwa kazi hiyo itakamilishwa katika
kipindi kilichokubaliwa. “Tunaweza kusema kuwa tunakaribia kumaliza
robo tatu ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.”
Profesa
pia amemwambia Rais Kikwete kuwa ni kweli wajumbe wa Tume hiyo wanakumbana na
watu ambao wanatumika kama kaseti za watu wengine. “Ni
kweli wapo. Mwanzoni walikuwa wengi lakini sasa tunaona kuwa wanaanza
kupungua.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es
Salaam.
30 Oktoba, 2012
Post a Comment