JKT RUVU.
KLABU ya
soka ya Polisi Moro SC imeendeleza kusuasu katika ligi kuu Tanzania bara
baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prinson katika
mchezo mkali na kusisimua liofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Dalili za
kupoteza mchezo huo zilianza mapema baada ya Prinson kutawala mchezo
dakika chache tangu kuanza na Polisi kuzinduka dakika ya tatu na
kujipatia bao la kuongoza lilifungwa na PaungoNywange kwa mkwaju wa
penalti.
Prinso
hawakukataa na kuendeleza mashambulizi na katika dakika ya 52 Peter
Michael aliisawazishia timu yake bao kwa njia ya mkwaju wa penalti na
kuongeza bao la pili katika dakika ya 77 baada ya walinzi wa Polisi Moro
kufanya uzembe wa kuondoa mpira katika eneo la hatari na kufungwa bao
hilo lililofungwa na Jhn Matei.
Katika
mchezo mungine Maafande wa Kujenga Ta4fa leo JKT Ruvu leo wamefanikiwa
kutoka na ushindi baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo na kuzuia
kujiuzulu kwa Kocha wake.
Kocha wa JKT Ruvu baada ya kufungwa na Azam FC goli 3 na kufikisha michezo mitatu wakipoteza alisema endapo angepoteza mchezo wa leo dhidi ya Mgambo Shooting uliochezwa leo katika uwanja wa Azam angejiuzulu.
JKT Ruvu wameifunga goli 1-0 Mgambo Shooting goli lililofungwa katika dakika 71 kupitia kwa Haruna Adolf na kuzidi kuwa weka mahali pabaya Mgambo Shooting iliyopoteza michezo yote mitano ya ligi hiyo.


Post a Comment