Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia alipofungua Mkutano wa kwanza
wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na
Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefunguliwa
leo Oktoba 15, 2012 katika Ukumbi wa AICC leo Oktoba 15 Jijini Arusha
na kuhudhuriwa na mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea barua ya wazi kutoka
kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai,
iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC) mara baada ya
kufungua Mkutano wa Kuhamasisha utalii barani Afrika leo, Oktoba 15,
2012, jijini Arusha. Katika Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mawaziri 17
kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wasanii wa ngoma ya
asili wa kabila la kimasai wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano
wa AICC jijini Arusha leo Oktoba 15, 2012 baada ya kufungua mkutano wa
kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na
Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Pakti ya kifuko cha unga wa Ubuyu
na kusikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya
Moringa Consultancy (TZ) Co Ltd, Christina Ngoti, wakati Makamu
alipokuwa akitembelea Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa
kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na
Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo
Oktoba 15, 2012 jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam wa
Tiba za Asili, James Kangaa, wakati Makamu alipokuwa akitembelea
Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa
wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii
Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 15, 2012
jijini Arusha. Picha na OMR
Post a Comment