Mwanajeshi mmoja amefariki
dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya ndege waliokuwa wakiirusha kuanguka
leo jijini Dar es Salaam.
Ndege hiyo ya Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWT) ilikuwa na marubani wawili na mmoja alifariki dunia
wakati akijaribu kuruka baada ya ndege hiyo kupata
hitilafu
wakati ikiwa hewani karibu
na eneo hilo.
Tukio hilo limetokea leo
katika kambi ya Jeshi la Anga, Ukonga jijini Dar es Salaam. Mwili wa mwanajeshi
aliyefariki umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es
Salaam.
Askari aliyejeruhiwa vibaya
katika ajali hiyo ni Kapteni Feruz Kwibika ambaye alipasuka kichwa na kulazwa
katika hospitali hiyo. Kwibika alijeruhiwa vibaya baada ya kuruka kutoka ndani
ya ndege hiyo kwa lengo la kuokoa maisha yake baada ya kutokea hitilafu
hiyo.
Wanajeshi hao walikuwa
kwenye mafunzo ya kawaida ambayo JWT wamekuwa wakifanya kwa ajili ya kuwajenga
vijana wa jeshi hilo.
Post a Comment