SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake,
Boniface Wambura ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa
mmoja wa maofisa watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za
Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika nchini Equatorial
Guinea.
Uteuzi
huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji
wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28,
2012 na kumalizika Novemba 11, 2012.
Wambura
atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali
hizo.
Wengine
ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka
Angola.
Wambura
atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo, kitu
ambacho TFF inajivunia kutoa mwakilishi kwenye moja ya mashindanoi makubwa ya
mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa
TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo
Wambura amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka
2011.
“Taarifa
zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe inang’ara CAF na hata FIFA kwa kuwa kwa
sasa wanajua kila kinachoendelea kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais Tenga na
kumtakia Wambura kila la kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa takriban siku
14.
Katibu
Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti, amemtakia
Wambura kazi njema na kwamba awe kioo cha mabadiliko makubwa yanayoendelea
kwenye soka la Tanzania.
Wambura
alijiunga na TFF Januari, 2011 akiwa mmoja wa waajiriwa watatu wapya kwenye
Shirikisho baada ya wsatendajiu wengine wawili kumaliza muda wao wa
mikataba.
Wambura
ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo
mbalimbali kuanzia kazi ya uandishi hadi Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo
ambalo alikuwa akifanya kazi kabla ya kujiunga na TFF.
Mahmoud
Garga (CAF)
Boniface
Wambura (Tanzania)
Arlindo
Macedo (Angola)



Post a Comment