Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino
Inmternational Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es
Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi wa Shindano la Redds Miss
Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria
Kimaro.
Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza zawadi ya Mshindi wa Taji la Reddds Miss Tanzania 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa
kampuni ya LINO AGENCY, Hashim Lundenga alisema katika fainali za shindano la
Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue
Pearl Hotel, (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni
shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania.
Leo hii
tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya Redds
Miss Tanzania mwaka zawadi zitakuwa kama
ifuatavyo
1)
Mshindi wa
Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
2)
Mshindi wa pili
atapata zawadi ya pesa taslimu shs:
6,200,000/-
3)
Mshindi wa tatu
atapata zawadi ya pesa taslmu shs:
4,000,000/-
4)
Mshindi wa nne
atapata zawadi ya pesa taslimu shs;
3,000,000/-
5)
Mshindi wa tano
atapata zawadi ya pesa taslimu shs:
2,400,000/-
6)
Mshindi wa sita
hadi wa 15 kila mmoja atapata shs:
1,200,000/-
7)
Washiriki
wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs:
700,000/-
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna
mashindano mengine madogo [Fast Tract] tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi
ya kuingia katika [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni Lucy
Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top
Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika
siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss
Talent.
Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss
Personality.
Nae
Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati
sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi
wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata tiketi
za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata burudani
mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana sana hasa
kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na sisi
kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi
wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu ni shindano la
kipekee.


Post a Comment