Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Nchini Tanzania Alberic Kacou kufuatia Umoja wa Mataifa kutimiza Miaka 67 tokea
kuasisiwa kwake. Pongezi hizo amezitoa Ofisini kwake katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja
wa Mataifa aliyepo Tanzania Bw. Alberic Kacou akizungumza na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif Ali Iddi
akisalimiana na Mwakilishi Mpya wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa
Mataifa Zanzibar Bibi Anna Senga.Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Nchini Tanzania Bwana Alberic Kacaou na kushoto kwa Balozi Seif ni Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum
Mohd.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza Umoja wa Mataifa (UN) kwa kutimia
miaka 67 tokea kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1945.
Balozi Seif ametoa pongezi
hizo wakati akisalimiana na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa
Maendeleo (UNDP) Ofisini kwake katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Ujumbe huo wa Shirika la
Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa ulioongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja
wa Mataifa aliyepo Nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou uliambatana pia na
Mwakilishi wa Shirika hilo aliyepo Zanzibar Bibi Anna Senga.
Balozi Seif amesema Umoja
huo umeundwa maalum kwa lengo la kutoa huduma itakayokidhi mahitaji ya Mataifa
yote Wanachama wa Umoja huo hasa katika masuala ya kustawisha Amani na ustawi wa
Jamii.
Ameeleza kwamba Taasisi
zilizoundwa chini ya mwavuli wa Umoja huo zimekuwa zikiendelea kutoa huduma
mbali mbali kwa Mataifa Wanachama zilizopelekea kupiga hatua kubwa za Maendeleo
hasa katika Nchi za Dunia ya Tatu.
Amesema Jamii za Kimataifa
zimekuwa zikishuhudia ufanisi huo hasa katika miradi ya Afya, Chakula na lishe,
Maji, sambamba na kudhamini Mafunzo ya Elimu ya Uraia kwa lengo la kutandika
Demokrasia Duniani.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar ameueleza Ujumbe huo wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa
Mataifa kwamba Zanzibar bado inahitaji kuendelea kuungwa mkono na Taasisi za
Umoja huo katika harakati zake za Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Amefahamisha kwamba mradi
wa huduma za maji safi na salama katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja
na Pemba umepewa kipaumbele katika jitihada za kuweka miundo
mbinu.
Mapema Mwakilishi Mkazi wa
Umoja wa Mataifa aliyepo Nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou alimueleza Balozi
Seif kwamba Umoja huo kupitia Mashirika yake ya Umoja huo (UNDP) yatajitahidi
kuendelea kuangalia mazingira ya kusaidia sekta ya Afya, Chakula na
Lishe.
Post a Comment