Mhe. Anna S. Makinda
(Mb) Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuongoza
Ujumbe wa Waheshimiwa Wabunge Wanne Kushiriki Mkutano na Jumuiya ya Umoja wa
Mabunge Duniani Inter - parliamentary Union (IPU) utakaofanyika mjini Qubec
nchini Canada kuanzia tarehe 21 – 26 Oktoba 2012 ikiwa ni sehemu ya kuimarisha
diplomasia ya kibunge (Parliamentary
Diplomacy).
Ujumbe huo wa
Waheshimiwa Wabunge utakaoshiriki Mkutano huo kutoka Tanzania ni pamoja
na:
- Mhe. Hamad Rashid Mohamed (Mb)
- Mhe. Susan L. Lyimo, (Mb)
- Mhe. David Kafulila (Mb) na
- Mhe. Dkt. Pudenciana kikwembe (Mb)
Agenda kubwa ya Mkutano
huu ni kulenga kuendeleza Mahusiano ya Mabunge Duniani katika kuchochea
maendeleo ya kiuchumi na kijamii sanjari na demokrasi ya kweli inayohusu mjadala
uliopewa jina la Uraia,
Utambulisho na Lugha, na Mtambuka wa Kuutamaduni katika Dunia ya
Utandawazi (Citizenship,
identify and linguistic and culture diversity in a globalized
world).
Pamoja na mjadala kuhusu
mada hii, Wabunge katika Jumuiya hiyo watajigawa katika kamati mbalimbali
kujadili masuala mbalimbali ya kibunge ambayo yamepewa mada
zifuatazo:-
- Enforcing the Responsibility to protect the Role of Parliament in Safeguarding civilians lives
- Fair Trade and innovative financing mechanism for sustainable development
- The use of media including social Media to enhance citizen engagement and democracy
Aidha taarifa ya Jumuiya
ya Umoja wa Mabunge Dunia (IPU) kuhusu mahusiano yake na umoja wa Mataifa
itatolewa kwa washiriki wa Mkutano huo ikifuatiwa na Mijadala mingineyo saba
amabayo itakuwa na maada zifuatazo:
- Mahusiano ya Nchi na nafasi ya diplomasia ya Kibunge(Multilateralism and the role of Parliamentary Diplomacy)
- Mahitaji Makubwa ya Mafuta: Nini Matarajio ya Usalama wa Nishati (Peak Oil: What prospects for energy security
- Ujengaji wa amani baada ya Migogoro (Building Peace after Conflict)
- kujenga fursa za Vijana katika uchumi wa kitandawazi(Creating Opportunities for youth in today’s global economy)
- Kinga za Kibunge: ni kwa manufaa au Mzigo?(Parliamentary immunity: benefit or burden?)
- Bunge na sheria za siasa, (Informal Panel: Parliamentary and political law)
- Warsha kuhusu nyenzo mpya za kuwezesha kupunguza matumizi ya nguvu za nuclear (Workshop on new tools to promote Nuclear disarmament).
Pamoja
na mijadala hiyo ujumbe wa Tanzania Utakutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo
Ndg. Anders
B. Johnsson na
kufanya mazungumzo ya pamoja kufuatia Tanzania kupewa heshima ya kuwa mwenyeji
wa kuandaa Semina ya Wabunge wanawake wa Jumuiya hiyo kutoka nchi za Afrika ya
mashariki, Afrika ya kati na kusini mwa Afrika.
Semina hiyo
itakayofanyika Tanzania itakuwa na mada kuhusu Mwitikio
na nmana ya kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake: kutoka Utungaji wa Sheria Husika
hadi kufika utekelezaji wake (Preventing
and Responding to violence against Women: From legislation to effective
enforcement) na itafanyika Dar – es- Salaam tarehe 5 – 7 Desemba 2012 ambapo
wajumbe zaidi ya 100 kutoka nchi 15 za SADC na Africa Mashariki watashiriki
.
Sambamba na Mkutano huo,
Makatibu wa Mabunge kutoka nchi wanachama watafanya vikao vitakavyo jadili
masuala mbalimbali ya kiutendaji ambapo katibu wa Bunge Dr. Thomas D.
Kashililah atawakilishwa na Ndugu Kileo Nyambele Mkurugenizi wa Maktaba na
Utafiti wa Bunge.
Ujumbe wa Tanzania
unatarajia kurejea nchini tarehe 28 Oktoba, 2012.
Imetolewa
na
Idara ya Habari, Elimu kwa
umma na Uhusiano wa Kimataifa
Dar es
salaam
17 Oktoba,
2012
Post a Comment