Injinia wa Manispaa ya wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Gerard Uriyo, amesema ujenzi wa barabara ya Kimara hadi King’ong,o unatarajiawa kuanza Oktoba 15 mwaka huu, na Kampuni ya Casco Costruction ndiyo itakayojenga .
Kauli hiyo imekuja baada ya diwani wa Kata ya Saranga, Efraimu Kinyafu kutoa siku saba za utekelezwaji wa barabara hiyo kinyume chake angewahamasisha wakazi wa eneo hilo kuandamana hadi kwa Mkurugezi wa Manispaa hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini jana,Uriyo alisema wakazi hao wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kuwa mchakato huo umekalika.
Uriyo alisema ujenzi wa barabara hiyo uanatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya kukamilika mchakato utiaji saini kati mkandarasi na manispaa hiyo hapo Oktoba 8 mwaka huu.
Alisema mkandarasi atakayesimamia ujenzi huo, na kampuni ya Casco Construction Limited ambapo mradi huo uatakamilika Machi 3, mwaka ujao.
Akifafanua zaidi, alisema Mradi huo utagharimu jumla ya sh milioni 281 ambapo wafadhili kutoka Japan wamechangia milioni 250, zilizobaki ni nguvu ya manispaa hiyo.
Alipoulizwa kuhusu hatua za kuanza kwa ujenzi huo, Diwani wa kata hiyo, Kinyafu, alisema hadi sasa hajapokea barua yeyote kuhusiana na ujenzi wa barabar hiyo.
Alisema ni aibu kwa Manispaa hiyo kwa kuwa haijawahi kutokea ikitekeleza miradi ya maendeleo ya katika kata hiyo bila wananchi kutumia nguvu ya maandamano jambo ambalo linatia shaka.
Post a Comment