DAR ES SALAAM, TANZANIA
Gazeti la
Mwananchi la leo katika habari yake iliyoongoza katika ukurasa wa kwanza,
limeandika kwamba, Sekretarieti Mpya ya CCM imepondwa kila kona, huku mmoja
watu mashuhuri waliohusishwa kuponda Sekretarieti hiyo akiwa ni Askofu Method
Kilaini. Kufuatia habari hiyo, Kilaini amekanusha habari hiyo. Nasi
tunaichapisha hapa kama tulivyoipata.
Kwa masikitiko
makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na
sekretariati ya CCM. Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na
wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lo lote
lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waugwana natumaini
watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa walikwazwa na hilo. Askofu
Kilaini
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
Post a Comment