Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UJENZI WA BANDARI MPYA BAGAMOYO WAZINDULIWA




TANZANIA imeingia makubaliano na Kampuni ya Ujenzi ya
(Merchants Holding Company), ya nchini China kwa ajili ya
ujenzi wa Bandari Mpya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji,Dk Mary
Nagu, alisema makubaliano ya awali yalifanyika
Septemba 5 mwaka huu.

Alisema ujenzi huo unaenda sambamba na uendelezaji wa
miradi mingine inayoambatana na ujenzi wa bandari hiyo
kwenye Eneo Maalumu
la kiuchumi la Bagamoyo (SEZ),

“Leo tunashuhudia uzinduzi rasmi wa kikosi kazi cha pamoja
kati ya serikali ya Tanzania na Kampuni ya China Merchants
Holding Company kitakachosimamia utekelezaji wa mradi huu”
alisema Dk Nagu.

Katika hilo, alieleza kuwa kikosi hicho kitasimamia miradi yote
itakayojumuisha ujenzi wa barabara itakayounganisha bandari
hiyo, mtandao wa barabara nyingine, pamoja na ujenzi wa Reli
itakayounganisha bandari hiyo na Reli ya kati na Tazara.

Aidha, alibainisha miradi hiyo itatekelezwa kwenye maeneo
maalumu na itatumika kama chachu ya maendeleo ya Taifa,
ikizingatiwa kwamba bandari hiyo itasaidia kupunguza msongamano
wa mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Akifafanua zaidi, Dk Nagu alisema jukumu hilo, linatokana na
Kaulimbiu ya Mkutano wa tano wa Mawaziri wa Nchi 50 za Kiafrika.

“Jukwaa hilo linaitwa ushirikiano wa nchi za Afrika na China
(FOCAC), ambao ndiyo chimbuko la mradi huu”alisema Dk Nagu.

Aliongeza kuwa mradi mpya utakuza kwa kiasi kikubwa ushindani
wa Tanzania Kikanda na Kimataifa kwa kuzingatia kwamba
utaongeza uwezo wa kuhudumia shehena za mizigo zinazoingia
na kwenda nchi ya Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Congo
(DRC), na Malawi.

Alitabanaisha kuwa mbali na maendeleo bado miradi hiyo
itaongeza mapato yatokanayo na biashara ya kimataifa,
kuongeza fursa za ajira jambo ambalo litachangia kiasi
kikubwa kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top