TAASISI ya ‘Rehema
Friendship and Solidarity’ , imekabidhi kisima cha
maji safi na salama kwa
wakazi wa Tegeta Dar es Salaam, kilichojengwa
kwa gharama sh milioni
7.3.
Kauli hiyo ilitolewa
jijini jana, na Mwenyekiti Mtendaji wa taasisi hiyo,
Abdi Adam Mohamed wakati
akikabidhi kisima hicho ambapo alisema
taasisi hiyo, kusaidia
jamii ya katika huduma mbalimbali muhimu.
Mohamed alisema kuwa
wamekuwa wakitoa misaada kwa jamii ikiwemo
ya elimu , afya na
huduma za maji safi na salama kwa kuchimba visima
na kukabidhi wa wananchi
bur bila malipo lakini wanafanya hivyo
baada ya kupokea maombi
ya eneo husika.
Alisema kisima hicho
ambacho wamekabidhi kwa wananchi wa Mtaa
wa Pwani na maeneo
jirani kinatarajia kusaidia zaidi ya watu 30,000
"Hadi sasa tumechimba na
kukabidhi visima zaidi ya 56 katika maeneo
mbalimbali nchini.Lengo
letu ni kuona Watanzania wananuifa na
uwepo wa taasisi yetu ya
Rehema ambayo ipo kwa ajili yao.
Tutaendelea kusaidia
jamii kadri tunavyoweza na katika maeneo
mengi zaidi.Tunafanya
hivyo pia katika kusaidia kwenye elimu na afya
,"alisema
Mohamed.
Hata hivyo alisema licha
ya kusaidia jamii katika upatikanaji wa
maji bado hawajawahi
kupata msamaha wa asilimia 10 ya kodi
kutokana na kazi hiyo na
kwamba kutokana na kuona umuhimu wa
maji wamekuwa
wakichimba visima bila ya kupewa msamaha na
Serikali.
Naye Katibu Tawala
Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, Bernard
Marcelline, wakati
akikabidhi kisima hicho alisema kuwa dhamira
ya Serikali ni kuona
wananchi wanapata maji safi na salama.
Alisema itakuwa jambo
jema kuona kinatunzwa na kutoa maji kwa
miaka mingi ijayo na
hiyo itatokana na wananchi wenyewe kuhakikisha
wanakitunza na
kukilinda.
Hata hivyo, alisema
hatarajii kusikia kuna mgogoro kutokana na
kuliwa fedha hizo na
kutumia nafasi hiyo kuwaasa kuwa waaminifu
na fedha ambazo zitakuwa
zinapatikana.
Post a Comment