Mhe. Balozi Radhia Msuya,
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini, akiwasha Mwenge,
ikiwa ni ishara ya kuadhimisha Sherehe za Kitaifa za Kutimiza Miaka Mia Moja ya
kuanzishwa kwa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini.
Sherehe hizo zilianza
katika vitongoji na miji kadhaa nchini Afrika Kusini tangu mwezi Januari 2012,
ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa walihudhuria, wakiwemo Mhe. Rais Jacob
Zuma ambaye alikuwa mgeni rasmi, Rais mstaafu Mhe. Benjamin W. Mkapa, pamoja na
marais na viongozi wa nchi mbali mbali.
Mjumbe wa Chama cha ANC,
Bw. Sochayile Khanyile, naye akiongea machache wakati wa Sherehe
hizo.
Mhe. Balozi Radhia Msuya,
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini akisema machache
wakati wa Sherehe za Mwenge za kuadhimisha Miaka 100 ya Chama Cha African
National Congress (ANC) zilizofanyika hivi karibuni tarehe 30 Oktoba,
2012 kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria, Afrika
Kusini.
Wanachama wa ANC
wakisikiliza hotuba ya Mhe. Balozi Msuya.
Wanajeshi wakiwa
wamejipanga kabla ya Sherehe rasmi za kuwasha Mwenge kuanza. Kushoto ni Bw.
Robert Kahendaguza, Mtawala Mkuu kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchi Afrika Kusini.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na Ubalozi wa Tanzania Nchini Afrika ya
Kusini
Post a Comment