|
|
|
|
Basi la Yanga |
Na Mahmoud
Zubeiry
BASI la
Yanga limefanyiwa fujo na watu wasiojulikana, wanaosadikiwa kuwa ni mashabiki wa
Simba, eneo la Kabuku, wakiwa njiani kuelekea
Tanga.
Baraka
Kizuguto, Ofisa tovuti wa Yanga aliye katika msafara wa timu ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba, jamaa aliyerushwa jiwe alikuwa juu ya mti na
limepasua kioo, ila halijajeruhi mtu.
Amesema
wametoa ripoti Polisi, ingawa hawakufanikiwa kumkamata mtu kwa sababu wahusika
walikuwa wamekwishakimbia baada ya tukio.
Yanga
iliyoondoka leo alfajiri Dar es Salaam tayari ipo Tanga , imefikia katika hoteli
ya Central City, barabara ya Nane na jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Gymkhana.
Yanga iko
Tanga kwa ajili mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga Jumapili.
Yanga
imepania kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo
wa Ligi Kuu, ambayo mzunguko wake wa pili utarejea Januari
mwakani.
Yanga
ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo,
Dar es Salaam jana na wachezaji wake wote wapo vizuri, chini ya kocha wake
Mholanzi, Ernie Brandts.
Wchezaji wa
Yanga wamepania kuvunja rekodi ya Coastal Union kutofungwa kwenye Uwanja wao wa
nyumbani, Mkwakwani, Tanga katika mechi hiyo.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY kwa niaba ya wenzake mapema wiki hii, Nahodha
Msaidizi wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ alisema kwamba wanataka
kustawisha uongozi wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwafunga
Coastal Jumamosi.
Alisema
wanajua Coastal ni timu nzuri na wanatarajiwa upinzani katika mechi hiyo, ila
ameonya Yanga ya sasa ni tishio na wachezaji wako vizuri ‘ile
mbaya’.
“Kwa kweli
mimi na wachezaji wenzangu tunamshukuru mwalimu mpya (Ernie Brandts) kwa kutupa
vitu vipya na muhimu. Timu yetu imebadilika na kila mtu anaona sasa. Wale
Coastal si hawafungwi kwao wale, sasa sisi tutaenda kuwafunga pale pale, tena
kipigo kikali,”alisema.
Lakini pia
habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba tayari wachezaji wameahidiwa donge
nono iwapo watashinda mechi hiyo.
Wachezaji
hao, walizawadiwa Sh. Milioni 15 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC
mwishoni mwa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo,
uliifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi
moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na
Simba SC yenye pointi 23, ambayo juzi imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini
Morogoro.
on Friday, November 9, 2012
Post a Comment