Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa yuko Ujerumani
ameeleza kusononeshwa kwake na habari za rushwa
zilizokithiri ndani ya CCM.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
jana, Lowassa alisema: “Nikiwa mwanaCCM na Mtanzania, ninasononeshwa sana na
taarifa za kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya chama chetu, serikalini na
katika taasisi mbalimbali.
“Ni kweli kwamba, rushwa ni tatizo. Ni kansa
ambayo kama taifa, hatuna budi kulitafutia ufumbuzi wa kimfumo badala ya
kuendelea kufikiri kwamba linaweza kumalizwa kwa njia ya kulalamika, kulaumiana
na kupakana matope.
“Tunao wajibu wa kuhakikisha kwamba Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inapewa meno na kuimarishwa zaidi katika
kukabiliana na vitendo hivi vya ukiukwaji wa maadili.”
Akizungumzia afya
yake Lowassa alisema: “Ninamshukuru Mungu siha yangu ni imara na kwamba
madaktari walionifanyia uchunguzi wamejiridhisha pasi na shaka kwamba afya yangu
ni njema.
“Ninaendelea na matibabu mazuri katika jicho langu moja ambalo
nilifanyiwa upasuaji miaka miwili iliyopita hapahapa, (Ujerumani), ninatarajia
kurejea nyumbani wakati wowote kuanzia sasa kuungana na Watanzania wenzangu
katika kulijenga taifa letu.”
Chanzo;Mwananchi
Burhan awekewa vikwazo na Marekani
6 hours ago
Post a Comment