Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

EPL CITY YASHINDWA RUDI KILELENI, BENITEZ APOKEWA NA MABANGO

 



Mabingwa watetezi Manchester City wakicheza huko Stamford Bridge dhidi ya Chelsea iliyokuwa na Meneja mpya Rafael Benitez akianza himaya kwa Mechi yake ya kwanza na kukaribishwa kwa kuzomewa na Mabango ya Mashabiki wasiomtaka walitoka sare 0-0 na kuwabakiza Manchester United kileleni wakiwa Pointi moja mbele ya City, walio nafasi ya 2, na Pointi 5 mbele ya Chelsea walio nafasi ya 4.
CHELSEA 0 MAN CITY 0
Uwanjani Stamford Bridge, katika Mechi ya kwanza ya Meneja mpya wa Chelsea Rafael Benitez, aliepokewa kwa kuzomewa na mabango ya kumpinga, Chelsea walitoka sare ya 0-0 na matokeo haya yamewafanya Manchester United wabakie kileleni.
VIKOSI:
Chelsea: Cech; Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole; Ramires, Mikel; Mata, Oscar, Hazard; Torres.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Barry, Y Toure, Silva, Milner, Dzeko, Aguero
Refa: Chris Foy
TOTTENHAM 3 WEST HAM 1
Bao mbili za Jermaine Defoe na moja la Gareth Bale leo zimewapa ushindi Tottenham wa Bao 3-1 walipocheza Uwanjani White Hart Lane na West Ham.
Bao la West Ham lilifungwa na Andy Carroll.
VIKOSI:
Tottenham Hotspur: Hugo Lloris, Steven Caulker, Jan Vertonghen, Kyle Walker, Michael Dawson, Sandro, Gareth Bale, Clint Dempsey, Aaron Lennon, Tom Huddlestone, Jermain Defoe
West Ham United: Jussi Jääskeläinen, Joey O'Brien, James Tomkins, Winston Reid, George McCartney, Modibo Maiga, Kevin Nolan, Mohamed Diamé, Gary O'Neil, Mark Noble, Andy Carroll
Refa: Andre Marriner
LIVERPOOL O SWANSEA CITY 0
Brendan Rodgers, Meneja wa Liverpool, leo alirudi Uwanja wa Liberty kucheza na Timu yake ya zamani Swansea City lakini akaambulia sare ya 0-0.
Jose Enrique wa Liverpool alifunga bao lakini lilikataliwa kwa kuwa Ofsaidi na shuti la Winga wao Raheem Sterling kugonga mwamba.
Nafasi bora ya Swansea ilimwangukia Ashley Williams ambae kichwa chake kiliokolewa na Joe Allen kwenye mstari wa goli.
Matokeo haya yamewainua Swansea na kukamata nafasi ya 8 na Liverpool wapo nafasi ya 11.
Hii ni Mechi ya 8 ya Ligi kwa Liverpool kutoka Uwanjani bila kufungwa na Swansea wamepoteza Mechi moja tu kati ya 7 walizocheza mwisho.
VIKOSI:
Swansea: Tremmel; Rangel, Williams, Chico, Davies; Routledge, Britton, de Guzman, Hernandez; Michu, Shechter.
Akiba: Cornell, Monk, Tiendalli, Agustien, Ki, Dyer, Lita.
Liverpool: Reina; Johnson, Skrtel, Agger, Enrique; Allen, Henderson, Gerrard; Downing, Sterling, Suarez.
Akiba: Jones, Carragher, Coates, Suso, Shelvey, Cole, Sahin.
Refa: Jon Moss
SOUTHAMPTON 2 NEWCASTLE O
Southampton wamejikwamua kutoka lile eneo denja la Timu 3 za mkiani ambazo hushushwa Daraja mwishoni mwa Msimu kwa kuichapa Newcastle Bao 2-0.
Bao za Southampton zilifungwa na Adam Lallana na Ramirez kupiga Bao la pili.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Simpson, Williamson, S. Taylor, Santon, Gutierrez , Tiote, Anita, Ferguson, Cisse, Ba
Akiba: Harper, Tavernier, Perch, Bigirimana, Marveaux, Sammy Ameobi, Ranger.
Southampton: Gazzaniga, Clyne, Fonte, Yoshida, Shaw, Puncheon, Schneiderlin, Cork, Lallana, Ramirez, Lambert
Akiba: K. Davis, Hooiveld, S. Davis, Rodriguez, Ward-Prowse, Mayuka, Guly.

msimamo umekuwa hivi baada ya mechi za leo
PositionTeamPlayedGoalDifferencePoints
No movement1Man Utd131430
No movement2Man City131529
No movement3West Brom13826
No movement4Chelsea131125
No movement5Everton13621
No movement6Arsenal131020
Moving up7Tottenham13120
Moving down8West Ham13119
Moving down9Swansea13217
No movement10Fulham13216
No movement11Liverpool13116
No movement12Stoke13016
No movement13Norwich13-915
No movement14Newcastle13-614
No movement15Wigan13-814
No movement16Sunderland12-412
Moving up17Southampton13-1011
Moving down18Aston Villa13-1210
Moving down19Reading12-69
No movement20QPR13-164
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top