Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi
Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal
akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono
wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini
hapo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib
Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la
msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab
Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said.
Mkuu wa mkoa wa Katavi
akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji
cha Kabungu.Msafara wa magari ya Makamu wa
Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi kwa
uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima cha kijiji cha Kabungu Mkoani
Katavi.
Wazee waasisi wa kijiji cha
Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama ishara ya kumpokea Makamu wa Rais
Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili katika kijiji hicho
leo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib
Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary
Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu
Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya
Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa
Katavi
Makamu wa Rais Dkt. Gharib
Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mkoa wa
Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia ni Waziri wa Uwezeshaji na
Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais
Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa
Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za
uzinduzi huo.
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea
na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na
wizara mbalimbali.
Waziri wa Ardhi na makazi
Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali
kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze
ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao
pia.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu
Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa
Katavi.
Kwaya ya Vijana ya Moravian
mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo uliofanyika kwenye viwanja vya
Kashaulili mjini Mpanda.
Martha Mbogo mwimbaji wa kundi
la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika
uzinduzi huo mjini Mpanda.
Wananchi wa Mpandawakinyanyua
mkono yao juu kama ishara ya kushangilia kuazinduliwa kwa mkoa wao wa Katavi
uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda
leo.
Watoto Daniel Ntwangile na
Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba
na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri
wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal
na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao
kuwatunza
Makamu wa Rais Dkt. Gharib
Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Veta Chuo cha Veta Mpanda
Trojemsi Bashato wakati alipotembelea banda la Veta.
Makamu wa Rais akisikiliza
maelezo kutoka kwa Thomas Lemunge mfanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wakati
alipotembelea Banda la kampuni hiyo, kulia ni Bw Huphrey Ngowi mmoja wa
wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal
akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa huduma Mwandamizi wa benki ya Wanawake TWB
BiMargaret Msengi wakati alipotembelea katika banda hilo
leo.
Makamu wa Rais Akizungumza na
wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea katika banda hilo leo njini
Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab
Rutengwe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa
wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda
leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wana Katavi wakati wa
uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini
Mpanda leo.
NA FULL
SHANGWE
Post a Comment