Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imetangaza kuwa fedha ilizopata kutokana na tuzo yake ya amani ya Nobel zitatolewa kusaidia watoto walioathirka na vita.
Kamisheni hiyo imetangaza uamuzi huo baada ya kukubaliana kuratibu fedha hizo taslimu kiasi cha euro 920,000 kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
Umoja huo ulichaguliwa mshindi wa tuzo hiyo kutokana na uwajibikaji wake katika masuala ya amani, demokrasia na haki za binaadamu kwa kipindi cha miaka 60 iliyopita.
Medali na cheti cha tuzo hiyo vitatolewa mjini Oslo, Norway katika hafla itakayofanyika tarehe 10 ya mwezi Desemba mwaka huu.