DAR ES SALAAM,
Tanzania
JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu
nchini, Fakihi Jundu, amemuapisha Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza,
Gaston Sanga kuwa Mjumbe wa Tume ya Polisi na
Magereza.
Akizungumza na wandishi wa
habari baada kumuapisha Kamshna huyo, Jaji huyo alisema tume hiyo imeundawa kwa
nujibu wa sheria za nchi kwa ajili ya kuteleleza majuku ya Idara hizo mbili,
ambapo kazi yake ni kusimamia nidhamu ya maofisa
wasaidizi
Jundu alisema kuapishwa kwa
Kamishna huyo kunafuatia baada ya wenzake wawili kuwapishwa Oktoba Mwaka huu,
huku yeye akiwa safarini Mkoani Mbeya.
“Mimi leo siyo msemaji
jaribuni kuzungumza naye Kamishna kile mnachohitaji”alisema Jaji
Jundu.
Naye Sanga alisema
tahakikisha anafanya kazi kwa uwadilifu ili tume hiyo iweze kuaminika miongoni
mwa maofisa wa Jeshi la Polisi na Magereza
nchini.
Alisema Tume hiyo imeundwa
mahususi kwa ajili ya kusimamia maslahi ya maofisa wa wa saidizi wa Idara hizo
mbili ikiwa ni pamoja na kusimamia upandishwaji vyo wa maofisa
hao.
Maofisa wengine wawili
Magereza ambao ni pamoja na Gerali John Minja na Kamshna wa sheria aktika ofisi
hiyo ya Magereza ,Juma Ally waliapishwa Otoba 30 mwaka huu.
Post a Comment