Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri
wa Elimu na Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, (wa pili kulia) wakikata utepe kwa
pamoja kuashiria kuzindua jengo jipya la Ofisi za Veta mkoa wa Mtwara na Lindi,
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa ajira kupitia mafunzo ya
Ufundi Stadi katika Chuo cha Ufundi cha VETA mkoani Mtwara. Hafla hiyo ya
uzinduzi imefanyika leo Nov 26, 2012 Mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Kanali Simba Kalia (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa VETA
nchini, Eng. Zebadia Moshi na (kulia) ni Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam,
Idrisa Msholo.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa VETA nchini, Eng. Zebadia
Moshi, wakati alipokuwa kitembelea kukagua jengo jipya la VETA lililopo Mkoani
Mtwara, baada ya kulizindua rasmi leo Nov 26, 2012. Wa pili (kushoto) ni Mke wa
Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa ajira kupitia
mafunzo ya Ufundi Stadi, Chuo cha Ufundi VETA mkoa wa Mtwara, leo Nov 26,
2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moham med Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha VETA, Lupakisa Mapamba,
kuhusu matumizi wa mashine ya kuchana mbao, wakati alipokuwa akitembelea katika
Karakana za Chuo hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa
ajira kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Chuo cha VETA, uliofanyika leo Nov 26,
2012 Mkoani Mtwara. Wa nne (kushoto) ni mke wa Makamu, Mama Zakhia
Bilal.
Post a Comment