Rais
Jakaya Kikwete akimuapisha Katibu
wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Winfrida Korosso mara baada ikulu jijini Dar es
Salaam, leo. (Picha
na Habari Mseto Blog)
Rais
Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria,
Winfrida Korosso mara baada ya kuapishwa kuwa katibu wa tume hiyo, Ikulu,
jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
wanafamilia
RAIS Jakaya Kikwete, leo
amewaapisha majaji wa mahakama kuu ya rufani, wajumbe wa tume ya uchaguzi na
katibu wa tume ya kurekebisha sheria, hafla iliyofanyika katika makazi ya Rais
Ikulu jijini Dar esSalaam.
Majaji walioapishwa kufanya
kazi katika mahakama ya rufani ni Bethel Makani na Ibrahim Khamis Jumaa,wakati
Jaji mstaafu John Mkwawa ameapishwa kuwa mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi,
huku Winnfrida Koroso, akiapishwa kuwa mjumbe wa tume ya kurekebisha
sheria.
Wakizungumza baada ya
kuapishwa kushika nafasi hizo wateule hao walisema watahakikisha wanafanya kazi
kwa uadilifu na moyo wa kujitolea kuhakikisha haki inatendeka katika nafasi
walizo nazo.
Makani alisema katika nafasi
yake hiyo mpya anayoenda kufanyia kazi kuna changamoto nyingi ikiwemo wananchi
kudhani suala la kucheleweshwa au kuahirishwa kwa kesi mbalimbali kunasababishwa
na mahakimu pamoja na majaji.
“Ni mara chache hakimu
kuahirisha kesi kama kutakuwa kila kitu kimekamilika nah ii hali ya kuchelewa
kwa kesi ina mzunguko mkubwa ikiwa ni pamoja na wananchi wenyewe kusdhindwa
kutoa ushirikiano na idara husikia katika kupata ukweli wa kufanyia
uamuzi”alisema Makani.
Kwaq Upande wake jaji John
Mkwawa alisema katika nafasi anayoenda kuhudumu changamoto zilizopo ni pamoja na
kufanyia marekebisho daftari la kudumu la wapiga kura iuli liendane na mahitaji
ya sasa ya watanzania.
Alisema changamoto nyingine
ni ucheleweshaji wa matokeo baada ya uchaguzi na kwamba hali hiyo inatokana na
kutokuwepo kwa teknolijia ya kisasa ya kuweza kufanyia kazi
hiyo.
Post a Comment