Diwani Gwae Mbua wa kata ya Mwankoko akimlalamikia mhandisi wa ujenzzi manispaa Singida Robert Massoro kwenye baraza la madiwani ktk ukumbi wa FDC na kufikia azimio la kumkataa
Mkurugenzi wa manispaa Singida, Mathias Mwangu akijibu hoja anazolalamikiwa mhandisi wa ujenzi Robert Massoro,kutoka kushoto ni naibu meya Hamisi Mkata, meya Salum Mahami na kulia kabisa ni DAS wa Singida Celestin Onditi..
Mkurugenzi wa manispaa Singida, Mathias Mwangu akijibu hoja anazolalamikiwa mhandisi wa ujenzi Robert Massoro,kutoka kushoto ni naibu meya Hamisi Mkata, meya Salum Mahami na kulia kabisa ni DAS wa Singida Celestin Onditi..
Pantaleo Sorongai, Diwani wa Mitunduruni akimlalamikia mhandisi wa manispaa Singida Robart Massoro kutokana na utendaji mbovu wa kazi zake
Na: Elisante John, Singida.
BARAZA la madiwani manispaa ya Singida limekataa kufanya kazi na mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo, Robert Masoro kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kugombana na wakandarasi, pia kutomudu usimamizi wa miradi ya ujenzi.
Azimio hilo lilifikiwa jana na baraza hilo, lililokutana kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini hapa.
Akitangaza azimio hilo, meya wa manispaa Singida, shekhe Salum Mahami alisema kutokanana tuhuma mbalimbali dhidi ya mhandisi Masoro, kwa pamoja baraza limeamua kutoendelea kufanya naye kazi kutokana na madhaifu mbalimbali.
“Baada ya baraza kubadilika na kukaa kama kamati ya baraza, injinia Masoro hahitajiki tena hapa…kumekuwa na matatizo na manyanyaso makubwa kati ya idara na wakandaras, madiwani wamekosa imani naye, suala hili halikuletwa hapa ili afufukuzwe kazi wala kusimamishwa kazi, bali imeleta pendekezo la kutohitahika tena katika manispaa yetu,”alisema Shekhe Mahami.
Baada ya baraza kusomewa taarifa hiyo, kwa pamoja madiwani wote waliunga mkono hoja hiyo, hivyo kumaanisha mhandisi Masoro hahitajiki tena katika manispaa ya Singida.
Awali baraza hilo lilielezwa kati ya sababu zilizopelekea mhandisi Masoro akataliwe kufanya kazia katika halmashauri hiyo ni, kushindwa kusimamia ujenzi wa daraja la Unyambwa kwa mwaka mmoja sasa, pia daraja la Mwankoko.
Madiwani hao wakiongozwa na Gwae Mbua, Shabani Sattu, Pantaleo Sorongai, Baltazar Kimario na Khadija Simba,walimshutumu wazi mhandisi huyo kutokana tuhuma mbalimbali, ikiwemo usimamizi mbovu ujenzi wa barabara ya Msufini, inayojengwa kwa lami.
Tuhuma zingine ni ujenzi duni wa barabara ya Peoples Club iliyogharimu zaidi ya Sh. Milioni 39, huku madaraja na mifereji ikiwa imejengwa chini ya kiwango.
Dosari zingine ni ujenzi wa miundo mbinu ya barabara (madaraja) na kutoa vibali ovyo vya ujenzi hata katika miradi ambayo yeye hahusiki, lakini akiwa na nia ya kuwekea mazingira fulani yanayokwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
Hata hivyo mhandisi huyo alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu kuhusiana na tuhuma hizo alidai kuwa hawezi kufanya kazi na watu wenye majungu na kwamba 'Singida siyo mwisho wa reli', anaweza kufanya kazi sehemu yoyote nchini, siyo lazima iwe Singida.
Post a Comment