Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
MSIBA wa msanii nyota wa
uchekeshaji hapa nchini, Hussein Mkiety, maarufu kama 'Sharomilionea' umegusa
hisia za wengi, huku King Majuto akikimbizwa Hospitali baada ya kushikwa na
presha, hivyo kutishia usalama wake.
Mtoto wa King Majuto, Hamza
Majuto, aliimbia HANDENI KWETU kuwa hali ya baba yake inaendelea vizuri kutokana
na kuumizwa zaidi na msiba wa Sharomlionea anayetamba katika ulingo wa filamu na
muziki hapa nchini.
Msanii huyo alikufa jana
saa mbili za usiku Maguzoni, kilimita chache na kijijini kwao Lusanga, wilayani
Muheza mkoani Tanga, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria lenye namba za
usajili T478 BVR Toyota Harrier kupinduka na kusababisha kifo
chake.
Kamanda wa Polisi mkoani
Tanga, Constantine Masawe, alikiri kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa mwili
wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule, Muheza, mkoani Tanga kwa taratibu
za mazishi zinazopangwa na familia yake.
“Marehemu alikufa majira ya
saa mbili za usiku kwenye barabara ya Segera alipokuwa anatoka Dar es Salaam
kwenda Muheza, hivyo mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule, huku
gari lake likihifadhiwa pia kwasababu haliwezi kutembea,” alisema
Masawe.
Taarifa za kifo cha msanii
huyo aliyeibukia hivi karibuni na kufanya vema katika ulingo huo zilianza
kuzagaa saa tatu za usiku, ikiwa ni dakika chache baada ya kufariki katika ajali
hiyo ya kusikitisha kwa nyota huyo.
Katika mitandao yote ya
kijamii kuanzia saa tatu za usiku zilizagaa habari zake, huku kila mmoja kiwa na
hisia tofauti zilizotokana na madai ya kifo cha msanii huyo, ambaye baadaye
jeshi la Polisi lilithibitisha kwa kupitia Kamanda wake,
Masawe.
Sharomilionea ameshacheza
filamu nyingi za uchekeshaji na kujipatia sifa kubwa, ikiwamo ile ya Sharo
Millionea, Imekula Kwako, Jini Mahaba, Porojo na nyinginezo zinazofanya vyema
katika tasnia ya filamu nchini.
Katika filamu ya Jini
Mahaba, Sharomillionea anayetamba pia kwa msemo wake wa ‘Umebug Men’, anacheza
kama mtu maarufu anayekwenda kujitambulisha kwa wake zake (Kingwendu) na
kushangazwa na hali zao za maisha.
Sharomillionea anamshangaa
mama yake mkwe anavyochambua mboga za majani wakati yeye sio utaratibu katika
maisha yake. “Huyu ndio mama yako Men? Mbona anachambua majani,” aliuliza huku
anakunja mdomo wake na kujifuta uso.
Maneno hayo yanamuumiza
mama yake mkwe na kuamua kumuita mume wake (Kingwendu) na kuja kushangaa
Sharobalo alivyokuwa katika mueneko wa super Star na kujikuta akipagawa
alipoanza kukejeliwa na mkwe wake.
Mbali na filamu hiyo ya
Jini Mahaba, mkali huyo pia ametamba katika filamu nyingi pamoja na nyimbo mbili
alizorekodi, huku pia akililiwa na wasanii wenzake kutokana na ushirikiano wake,
mara baada ya kuibuka kisanii.
Wasanii wengi
waliozungumzia kifo cha Sharomillionea wakiongozwa na Steve Nyerere,
walionyeshwa kuchanganyikiwa kwa msiba wa msanii aliyeanza kutokea peupe na
kutamba mno katika sanaa ya uchekeshaji.
Sharomillionea
aliyetokea katika ubavu wa nguli wa vichekesho nchini, King Majuto, anazikwa
kesho Jumatano, kijijini kwao Lusanga, huku wasanii wengi wakitarajia kuhudhuria
msiba na mazishi ya nyota huyo aliyeipenda pia nyumbani kwao Muheza.
Post a Comment