Wanajeshi wa Serikali ya Libya.
AFISA mmoja mkuu
wa usalama nchini Libya amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake mjini
Benghazi.
Wizara ya usalama
wa ndani nchini humo imeelezea kuwa Bwana Farraj al-Dursi , ambaye alikuwa mkuu
wa polisi mjini humo, amefariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya
kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Kumekuwa na visa
vingi vya mauji mjini Benghazi katika siku za hivi punde.
Mnamo mwezi
Septemba, balozi wa marekani mjini Benghazi aliuawa pamoja na wamarekani watatu
katika ubalozi huo.
Col Dursia
aliteuliwa kuwa mku wa polisi mjini humo muda mfupi baada ya shambulio
lililotekelezwa kwenye ubalozi wa Marekani, ambalo balozi wa Marekani na maafisa
watatu waliuawa.
Maafisa kadhaa wa
Ulinzi wameuawa na watu wasiojulikana mjini Benghazi, mji ambao maandamano na
machafuko yaliyomuondoa madarakani Muamarr Gaddafi yalianza.
Mwandishi wa BBC
mjini Tripoli, anasema wengi wa maafisa hao wanalengwa kwa sababu wanakisiwa
kuwa na uhusiano na serikali ya ya zamani ya nchi hiyo.
Kabla ya
serikali, ya Gadaffi kuondolewa madarakani, Kanali, Dursi alifahamika kuwa afisa
aliyehusika na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya.
Post a Comment