Washiriki
wa EBSS Salma Yussuf Abushir, Nsami Nkwabi, NshomaNghangasamala, Walter Chilambo
na Wababa Mtuka wakiwa na Ritha Poulsen. Je, nani ataondoka na kitita cha Sh.
Milioni 50 kesho?
|
Na Bin Zubeiry
BAADA ya
miezi mitatu ya mchuano mkali hatimaye mshindi wa shindano la kuimba la Epiq
Bongo Star Search atapatikana leo katika fainali kali inayofanyika katika ukumbi
wa Diamond Jubilee.
Mshindi
atajinyakulia shilingi milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi kutoka kwa
wadhamini pekee wa shindano hilo kampuni ya simu za mikononi ya
Zantel.
Washiriki
walioingia kwenye fainali hizo ni EBSS06: Nsami Nkwabi, EBSS07: Nshoma
Ng’hangasamala, EBSS09: Salma Abushiri, EBSS11: Wababa Mtuka (Dar) na EBSS12:
Walter Chilambo (Dar).
Wasanii
watakaoburudisha ni Rich Mavoko, Omi Dimpoz, Ben Paul, Lina, Amini, Mzee Yusuf,
Haji Ramadhan, Mwasiti, Ditto, Laila Rashid, Linex na Barnaba.
Akizungumzia
fainali hizo, jaji mkuu wa shindano hilo, Madam Ritha Paulsen, aliwashukuru
watanzania kwa ushirikiano waliowapa toka shindano limeanza mpaka leo
wanahitimisha kwa fainali.
‘Kama
mlivyoona shindano hili toka lilipoanza mwaka huu limekuwa la kimataifa zaidi,
hivyo tarajieni fainali za kipekee na zitakazoweka rekodi kwenye tasnia ya
burudani na ni matarajio yetu kwamba mshindi wa usiku huu atafanya vizuri kwenye
muziki’ alisema Madam Ritha.
Kwa upande
wake Afsa Biashara mkuu wa Zantel, bwana Sajid Khan alisisitiza utayari wa
kampuni yake katika kuwaendeleza vijana wa kitanzania kufikia ndoto zao lakini
aliomba pia wadau wengine wa sanaa kuwapa washirikiano washiriki
wote.
‘Zantel,
pamoja na kumpa mshindi zawadi ya milioni hamsini lakini pia tutampa mkataba wa
kurekodi, na washiriki wengine watapewa nafasi ya kurekodi wimbo mmoja mmoja
lakini juhudi hizi zitafanikiwa ikiwa tutapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa
wadau’ alisema Khan.
Shindano
hilo limekuwa likirushwa hewani na kituo cha runinga cha ITV, lilianza mwezi wa
sita kwa kufanya usaili mikoani, ambalo mwaka huu lilienda mikoa nane-Mbeya,
Dodoma, Mwanza, Tanga, Dar es Salaam, Zanzibar, Lindi pamoja na
Arusha.
Kwa mara ya
kwanza pia shindano hilo liliweza kufanya usaili kwa njia ya simu ili kuwapa
nafasi vijana zaidi ambao hawakufikiwa na majaji.
Epiq Bongo
Star Search ni kipindi cha televisheni ambacho huibua vipaji vya muziki kwa
vijana wa kitanzania na kinatengenezwa na Benchmark Productions, na toka
kimeanzishwa mwaka 2006 kimekuwa ni kipindi kinachotazamwa zaidi Afrika
mashariki kwa kufikisha watu milioni 3 wanaotazama kwa kila
kipindi.
Mwaka huu
kinadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, na mshindi atapata
zawadi ya shilingi milioni 50 pamoja na mkataba wa kurekodi.
Post a Comment