Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania
Mudhihili Mudhihili (kulia) akiwaandikia waandishi wa habari jina lake
wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar
es Salaam. Katika mkutano huo mambo mbalimbali yaliongelewa ikiwa ni pamoja na
bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa shilingi 1200 kwa
daraja la kwanza na 960 kwa daraja la pili.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Mudhihili Mudhihili (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es
Salaam kuhusu bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa
2012/2013 kuwa shilingi 1200 kwa daraja la kwanza na 960 kwa
daraja la pili. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa bodi ya Korosho Tanzania
Theofora Nyoni.
Baadhi ya waandishi wa
habari waliohudhulia mkutano baina yao na bodi ya korosho uliofanyika leo katika
ofisi za bodi hiyo jijini Dar es Salaam wakijitahidi kupata matukio muhimu ya
mkutano huo. Katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania
Mudhihili Mudhihili (hayupo pichani) alisema kuwa bei ya mkulima ya kununulia
korosho msimu wa mwaka 2012/2013 ni shilingi 1200 kwa daraja la kwanza na 960
kwa daraja la pili.Picha na Anna Nkinda –
Maelezo
Post a Comment