WAFUGAJI
WAKISUBIRI MALORI ILI KUWEZA KUPAKIA MIFUGO YAO KATIKA ENEO LA MIKUMI IFAKARA
WAKATI WA ZOEZI LA UHAMAJI WA HIYARI KATIKA HIFADI YA BONDE LA MTO KILOMBERO
WILAYA YA KILOMBERO HIVI KARIBU.MAKUNDI ya wafugaji
wameanza kuondoka maeneo ya wakulima katika mji wa Ikwiriri walipokuwa wakiishi
kwa muda mrefu tangu mwaka 2007, walikokaribishwa na viongozi wa vijiji na
vitongoji.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu alisema jana kuwa
wafugaji hao walikuwa wakiishi kinyume cha sheria kwa kwamba, maeneo hayo
hayakutengwa kwa ajili ya wafugaji.
Babu baada ya kuingia wilayani Rufiji, amekumbana na
changamoto ya wafugaji hao ambao walitakiwa kuhama maeneo hayo na kumekuwa
kukiripotiwa mapigano ya mara kwa mara kati ya wakulima na
wafugaji.
Alisema wafugaji hao wametengewa maeneo ya Tawi,
Mbwara, Chumbi A, B na C wameonekana wakiswaga mifugo yao kuelekea kwenda
kupakia magari kwa ajili ya usafirishaji.
“Wamekuja ofisini kwangu na wameniomba kibali cha
kusafirisha mifugo, nami nimekubali bila pingamizi,” alisema.
Babu alisema hata
kwa wale wanaotaka kupitisha mifugo kupitia daraja la Mkapa watapata kibali
kutoka ofsi yake.
Alisema maeneo ambayo hayana maji wamekubaliana na
wafugaji hao kuwa waende kwanza, halafu jitihada za kutengeneza miundombinu ya
maji na malambo itaendelea bila tatizo jambo la msingi ni kuhama
kwanza.
Alirudia kauli yake kuwa wanaotakiwa kuhama ni
wafugaji wanaoishi katika Tarafa ya Ikwiriri na kwamba, wengine waliopo katika
tarafa nyingine waendelee kubaki.
Kuondoka kwa wafugaji katika eneo hilo kumeondoa pia
tishio la wananchi wa Tarafa ya Ikwiriri, kufanya maandamano kushinikiza
kuondoka kwa wafugaji hao.
Post a Comment