Mwandishi wa Habari wa
gazeti la Tanzania Daima,Charles Ndagula akiwa amelazwa kwa ajili ya matibabu
kwenye hospitali ya St Joseph iliyopo Mjini Moshi baada ya kunusurika kuuawa kwa
kugongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafayabiashara wa kusfirisha sukari ya
magendo kwa njia za panya kwenda nchini Kenya, Picha na Rodrick
Mushi.
WAFANYABIASHARA wanaosafirisha sukari kwa magendo
kwenda nchini Kenya, juzi walifanya jaribio la kumuua mwandishi wa habari wa
gazeti la Tanzania Daima mkoani Kilimanjaro, Charles
Ndagulla.
Tukio hilo lilitokea saa 6:00 usiku, baada ya
wafanyabiashara hao wakiwa na gari aina ya Toyota RAV 4J, kumgonga kwa makusudi
mwandishi huyo na kufanikiwa kuvusha malori mawili yakiwa na
sukari.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ambalo
limeibua maswali mengi, kuhusu kiburi cha wafanyabiashara hao hadi wafikie hatua
ya kutaka kutoa uhai wa mwandishi ili kutimiza malengo yao.
Kabla ya waandishi wa habari za uchunguzi kwenda eneo
la Holili karibu na machimbo ya madini ya Pozorana, walidokezwa kuwa malori 12
aina ya Fusso yangevuka mpaka usiku kwenda Kenya.
Malori hayo yalikuwa yaanzie safari zake mji wa Himo na
kuelekea barabara ya Himo-Holili, kisha yangechepuka na kushika barabara ya
Lower Rombo hadi eneo hilo la madini na kuingia Kenya.
Mpaka waandishi wa habari wanafika eneo ulipotokea
mkasa huo, tayari malori sita yalikuwa yameshavuka mpaka kupitia njia za panya
eneo la Holili kati ya saa 4:00 na saa 5:00 usiku huo.
Lakini, kabla ya waandishi wa habari kwenda eneo hilo,
walimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz ambaye aliahidi
kuwaandaa polisi kwa lengo la kukamata malori hayo.
Baada ya kufika eneo hilo, malori hayo yalijitokeza na
waandishi waliyasimamisha na madereva wake kutii amri hiyo, Mwandishi wa habari
hizi alimtaarifu Kamanda Boaz muda huohuo.
Pia, mwandishi wa habari hizi alimtaarifu Meneja wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Patience Minga ambaye
aliahidi kutuma maofisa wake wa doria.
Lakini wakati waandishi wakisubiri msaada wa polisi,
ilifika gari ndogo aina ya RAV 4J ikiwa na watu wawili mmoja mwanamke, ambao
waliwaamuru madereva hao kuondoa kwa nguvu malori hayo.
Mwandishi wa Tanzania Daima ambaye alikuwa upande wa
yalipokuwa yakielekea malori hayo, aliwamulika kwa tochi watu waliokuwa katika
gari ndogo ndipo walipomfuata na kumgonga.
Post a Comment