Rais
Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa
hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata
muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu
ya White House.
Mwandishi wa BBC ambaye
yuko kwenye kampeini ya Romney, anasema kuwa hizi dakika za mwisho ni kuhusu
kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi huu wenye ushindani mkali
Kura za kwanza zimepigwa
katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura
tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa
ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana
kama Electoral village.
Chanzo - BBC
Swahili
Post a Comment