Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo
cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga baada ya
kuwasili kwenye Kanisa la Mama wa Huruma katika Parokia ya Ngokolo mjini
Shinyanga kushiriki mazishi ya Askofu huyo leo, Jumamosi, Novemba 10,
2012.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
Mhashamu Baba Askofu Aloysious Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa
mazishi wa Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga
leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la
Askofu Aloysius Balina wakati wa mazishi ya Askofu huyo leo kwenye Kanisa la
Mama wa Huruma, mjini Shinyanga.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada
la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga
wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo,
Shinyanga leo. Picha na mdau Fred Maro wa Ikulu
Post a Comment